Friday, April 29, 2022
Thursday, April 28, 2022
MAMLAKA YA MJI WA BUSAN KUSAIDIA KUENDELEZA UCHUMI WA BLUU NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokelewa na mwenyeji wake Mstahiki Meya wa Mji wa Busan Mhe. Park Heong Joon alipowasili ofisini kwake. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mstahiki Meya wa Mji wa Busan, Korea Mhe. Park Heong Joon wakifurahia jambo walipokutana kwa mazungumzo |
Mazungumzo yakiendelea |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Liberata akimkabithi picha ya wanyama wa mbugani (yakuchorwa) Mstahiki Meya wa Mji wa Busan, Korea Mhe. Park Heong Joon |
Wednesday, April 27, 2022
WIZARA YA MAMBO YA NJE YAJIPANGA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WAKE
Na Waandishi wetu, Dodoma
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imejipanga kuwajengea uwezo wa kazi watumishi wake ili kuwawezesha kutekeleza kwa vitendo Diplomasia ya Uchumi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Joseph Sokoine wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Jijini Dodoma
“Tumekuwa na kikao cha Baraza la Wafanyakazi kama ilivyo kwa mujibu wa Sheria, kikao kilijadili pamoja na mambo mengine, bajeti ya Wizara kwa mwaka mpya wa fedha 2022/2023, kuboresha utendaji kazi wa Wizara pamoja na maslahi ya watumishi.
“Katika masuala tuliyojadili leo katika kuboresja maslahi ya wafanyakazi ni pamoja na eneo la mafunzo ili kuendelea kuwajengeauwezo watumishi wetu wa kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo,” amesema Balozi Sokoine
Kwa upande wake Katibu wa TUGHE ngazi ya Taifa, Bw. Amani Msuya ameupongeza uongozi wa Wizara kwa kuyapa kipaumbele maslahi ya watumishi na kuwataka Watumishi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa bidii na maarifa yote kwa maslahi mapana ya Taifa.
Naye Mwenyekiti wa TUGHE wa tawi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Pilly Sukwa amesema kuwa kikao cha baraza kimejadili masuala ya Bajeti pamoja umuhimu wa kuboresha zaidi maslahi ya watumishi wa Wizara ili kuwaongezea morali ya kazi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa tija na ufanisi zaidi.
“Katika eneo langu mimi kama mwenyekiti wa TUGHE hapa Wizarani ni kuhakikisha kuwa maslahi ya watumishi ikiwemo mishahara na maslahi mengine yamezingatiwa. Ninaishukuru Wizara mambo yote haya yamezingatiwa wakati wa mkutano huu wa Baraza,” amesema Bi. Sukwa.
Baraza la Wafanyakazi wa Wizara limefanyika kwa lengo kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2021/2022 na Makadirio ya Makisio ya Bajeti kwa Mwaka 2022/2023.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab naye akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara. |
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Pilly Sukwa akizungumza wakati wa Mkutano huo wa Baraza la Wafanyakazi |
Katibu wa TUGHE ngazi ya Taifa, Bw. Amani Msuya naye akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Sokoine (katikati walioketi) akiwa katika picha na Ssehemu ya Wajumbe wa Baraza hilo |
Picha ya pamoja |
Picha ya pamoja |
Mjumbe wa Baraza ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, Bw. Magabilo Murobi akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi |
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Abel Maganya naye akichangia hoja wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi. |
Tuesday, April 26, 2022
JAMHURI YA KOREA YAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI
Balozi wa Tanzania nchini Korea Mhe.Togolani Mavula akifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea |
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Caesar Waitara akifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea |
Mazungumzo yakiendelea |
TANZANIA KUENDELEA KUULINDA MUUNGANO ILI KUWAENZI WAASISI WAKE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango amewataka watanzania kuendelea kuwaenzi waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuulinda, kuuheshimu na kuusherehekea kwa kuwa una manufaa makubwa kwao ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
Mhe. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa maadhimisho ya Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na wananchi kwa ujumla.
Mhe. Dkt.
Mpango ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan kwenye sherehe hizo amesema kuwa, Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ambao waasisi wake ni Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ni tunu ya taifa inayotakiwa kulindwa, kuheshimiwa na kusherehekewa
kwani amani, umoja, usalama na mshikamano uliopo miongoni mwa watanzania
unatokana na Muungano huo.
Pia, ameongeza
kusema kuwa, mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 58 ni mengi na ya
kujivunia katika sekta zote za uchumi, utamaduni, siasa, elimu na ajira.
“Tutaendelea
kuulinda Muungano wetu kwani una manufaa makubwa kwetu sisi kama taifa moja. Tunaposherehekea
miaka 58 ya Muungano tunayo mengi ya kujivunia, biashara kati ya Watanzania
imeimarika, raia wetu wanaweza kuishi popote bila tatizo lolote tuna amani na
utulivu unaowawezesha wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi na kijamii
bila kikwazo chochote, alisema Mhe. Dkt. Mpango.
Halikadhalika
Mhe. Mpango amesema kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ni wa kipekee
duniani, umeendelea kuijengea heshima Tanzania tangu enzi za kupigania ukombozi
wa Nchi za Kusini mwa Afrika hadi sasa.
“Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imeendelea kuheshimika duniani kutokana na mchango wake
kwenye medani za kimataifa. Tangu harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa
Afrika Tanzania ilikuwa mstari wa mbele hadi sasa Tanzania imeendelea kuchangia
vikosi vya kulinda amani kwenye nchi mbalimbali duniani na kushiriki kwenye
usuluhishi wa migogoro. Tanzania itaendelea kunufaika kama nchi moja na fursa
zote zinazotokana na mashirika ya kikanda na kimataifa ikiwemo SADC, EAC na Soko
Huru la Biashara Huru barani Afrika “aliongeza kusema Mhe. Dkt. Mpango.
Wakati wa
Maadhimisho hayo, Makamu wa Rais alizindua Kitabu Maalum cha Historia ya Muungano ambacho aliagiza kisambazwe kwenye Shule, Vyuo na Taasisi mbalimbali
ili kuwawezesha wananchi hususan vijana kuuelewa Muungano.
Awali
akizungumza kumkaribisha Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema maadhimisho ya mwaka 2022 ambayo ni ya
kipekee yataambatana na midahalo na makongamano ya uelimishaji kuhusu Muungano
ili kuhakikisha kila Mtanzania hususan vijana wanauelewa Muungano ambao ni tunu
na urithi wa Wanzania.
Aidha,
akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdula amesema Mhe. Rais Mwinyi ameahidi
kuendelea kuusimamia na kuulinda Muungano kwa nguvu zake zote na kwamba
Muungano upo salama kwenye mikono yake na ya Mhe. Rais Samia.
Kwa upande
wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Muungano na
Mazingira, Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa Muungano upo salama na kwamba tayari
kero za Muungano 18 kati ya 25 zimetatuliwa.
Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambayo ni moja ya Wizara za
Muungano imeshiriki maadhimisho hayo yenye kaulimbiu isemayo ““Miaka 58 ya Muungano: Uwajibikaji na Uongozi
Bora; Tushiriki Sensa ya Watu na Anuani ya Makazi kwa Maendeleo Yetu”.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa sherehe za miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika jijini Dodoma tarehe 26 Aprili 2022 |
Sehemu ya Mabalozi na Wakuu wa Mashirika waliopo nchini wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. |
Sehemu nyingine ya washiriki kutoka Wizarani wakiwa kwenye maadhimisho hayo. |
Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mpango akizindua kitabu maalum cha historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. |
Mhe. Makamu wa Rais akimkabidhi nakala ya kitabu mwakilishi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania |
Mhe. Makamu wa Rais akimkabidhi Mzee Hasanieli Mrema nakala ya kitabu. Mzee Mrema ni mmoja wa wazee waliochanganya mchanga kuashiria kuasisiwa kwa Muungano |
Mhe. Balozi Mbarouk akifurahia jambo na Balozi Fatma mara baada ya maadhimisho kumalizika |
Mhe. Balozi Mbarouk kwa pamoja na Balozi Fatma wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara walioshiriki maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanzania |
Picha ya pamoja |
Monday, April 25, 2022
WAZIRI MULAMULA ZIARANI NCHINI KOREA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Dkt. Aboud S. Jumbe akifafanua jambo kwenye ziara ianayoendelea Jamhuri ya Korea. |