Friday, May 17, 2024

ETHIOPIA YAFUNGUA NJIA UJENZI WA UBALOZI DODOMA

Serikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia katika Mji wa Serikali Dodoma ya kuwa nchi ya kwanza kujenga majengo ya Ofisi na Makazi ya Balozi na kuzitolea wito nchi nyingine kuiga mfano huo.

 

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethipia, Mhe, Birtukan Ayano ambapo kwa pamoja waliweka Jiwe la Msingi la ujenzi huo kwa niaba ya Serikali zao katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma leo Mei 17, 2024.

 

Balozi Mbarouk alieleza kuwa uwekaji wa jiwe la msingi huo ni kielelezo tosha cha kuimarika kwa ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Ethiopia ambao ulianza tangu enzi za waasisi wa mataifa haya, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Haile Selassie.

 

Balozi Mbarouk alisisitiza umuhimu wa kukuza biashara baina ya nchi hizi mbili kwa kuwa kiwango cha biashara kinachofanyika hivi sasa hakiakisi uhusio mzuri uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

 

Kwa upande wake, Mhe. Ayano alisema uwekaji wa jiwe la msingi huo ni ishara ya ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili na dhamira ya dhati ya Serikali ya Ethiopia ya kuuimarisha zaidi, hususan katika nyanja ya biashara na uwekezaji.

 

Hafla ya uwekaji jiwe la msingi ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule ambapo aliwahakikishia jumuiya ya wanadiplomasia nchini kuwa Dodoma ipo tayari kuwapokea na miundombinu ya kijamii ikwemo maji, elimu, afya na usafirishaji, Serikali inaendelea kuijenga na kuiboresha iliyopo. 

 

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga; Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vicent Mbogo, Naibu Katibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa, Meya wa Halimashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe na viongozi waandamizi wa Serikali

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Mhe. Balozi Birtukan Anayo wakifungua kitambaa kuonesha jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma baada ya kuweka jiwe hilo huku wakishuhudiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy Nderiananga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama na viongozi wengine wa Chama na Serikali.
 
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Mhe. Balozi Birtukan Anayo wakionesha jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma baada ya kuweka jiwe hilo huku wakishuhudiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy Nderiananga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama Mhe. Vicent Mbogo na viongozi wengine wa Chama na Serikali. 
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Balozi wa Ethiopia nchini Tanzania Mhe. Shibru Memo Kadida akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma
 
Wajumbe wa Meza kuu wakifuatilia hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa (kushoto) na Meya wa Jiji la Dodoma prof. Davis Mwamfupe wakifuatilia hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama Mhe. Vicent Mbogo, (kulia) Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (wa pili kulia)  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy Nderiananga (katikati) Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Balozi Birtukan Ayano na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakimsikiliza mtaalamu wa kampui iiyoandaa mchoro wa jengo la Ubalozi wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Mhe. Balozi Birtukan Anayo katika picha ya wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma baada ya kuweka jiwe hilo wengine ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy Nderiananga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama na viongozi wengine wa Chama na Serikali.

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Mhe. Balozi Birtukan Anayo katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma baada ya kuweka jiwe hilo huku wakishuhudiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy Nderiananga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama na viongozi wengine wa Chama na Serikali.

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) akiagana na Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Mhe. Balozi Birtukan Anayo baada ya kukamilika kwa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma baada ya kuweka jiwe hilo huku wakishuhudiwa na Balozi wa Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa.

 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.