Serikali
ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia katika Mji wa
Serikali Dodoma ya kuwa nchi ya kwanza kujenga majengo ya Ofisi na Makazi ya
Balozi na kuzitolea wito nchi nyingine kuiga mfano huo.
Pongezi
hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa
Ethipia, Mhe, Birtukan Ayano ambapo kwa pamoja waliweka Jiwe la Msingi la
ujenzi huo kwa niaba ya Serikali zao katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma
leo Mei 17, 2024.
Balozi
Mbarouk alieleza kuwa uwekaji wa jiwe la msingi huo ni kielelezo tosha cha
kuimarika kwa ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Ethiopia ambao
ulianza tangu enzi za waasisi wa mataifa haya, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere na Hayati Haile
Selassie.
Balozi
Mbarouk alisisitiza umuhimu wa kukuza biashara baina ya nchi hizi mbili kwa
kuwa kiwango cha biashara kinachofanyika hivi sasa hakiakisi uhusio mzuri
uliopo baina ya mataifa hayo mawili.
Kwa
upande wake, Mhe. Ayano alisema uwekaji wa jiwe la msingi huo ni ishara ya
ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili na dhamira ya dhati ya
Serikali ya Ethiopia ya kuuimarisha zaidi, hususan katika nyanja ya biashara na
uwekezaji.
Hafla
ya uwekaji jiwe la msingi ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.
Rosemary Senyamule ambapo aliwahakikishia jumuiya ya wanadiplomasia nchini kuwa
Dodoma ipo tayari kuwapokea na miundombinu ya kijamii ikwemo maji, elimu, afya
na usafirishaji, Serikali inaendelea kuijenga na kuiboresha iliyopo.
Viongozi
wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe.
Ummy Nderiananga; Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vicent Mbogo, Naibu Katibu wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa, Meya wa Halimashauri
ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe na viongozi waandamizi wa Serikali
|
Naibu Waziri Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor
Mbarouk akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Mhe. Balozi Birtukan
Anayo wakifungua kitambaa kuonesha jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika
mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma baada ya kuweka jiwe hilo huku
wakishuhudiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy
Nderiananga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa
Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida, Makamu Mwenyekiti Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama na viongozi wengine
wa Chama na Serikali.
|
|
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Mhe. Balozi Birtukan Anayo wakionesha jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma baada ya kuweka jiwe hilo huku wakishuhudiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy Nderiananga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama Mhe. Vicent Mbogo na viongozi wengine wa Chama na Serikali.
|
|
Naibu Waziri Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor
Mbarouk akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika
mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika
mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. |
|
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika
mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. |
|
Balozi wa Ethiopia nchini Tanzania Mhe. Shibru Memo Kadida akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika
mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma |
|
Wajumbe wa Meza kuu wakifuatilia hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika
mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. |
|
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa (kushoto) na Meya wa Jiji la Dodoma prof. Davis Mwamfupe wakifuatilia hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika
mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. |
|
Makamu Mwenyekiti Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama Mhe. Vicent Mbogo, (kulia) Naibu Waziri Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor
Mbarouk (wa pili kulia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy
Nderiananga (katikati) Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Balozi Birtukan Ayano na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakimsikiliza mtaalamu wa kampui iiyoandaa mchoro wa jengo la Ubalozi wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. |
|
Naibu Waziri Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor
Mbarouk akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Mhe. Balozi Birtukan
Anayo katika picha ya wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika
mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma baada ya kuweka jiwe hilo wengine ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy
Nderiananga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa
Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida, Makamu Mwenyekiti Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama na viongozi wengine
wa Chama na Serikali. |
|
Naibu Waziri Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor
Mbarouk akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Mhe. Balozi Birtukan
Anayo katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika
mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma baada ya kuweka jiwe hilo huku
wakishuhudiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Ummy
Nderiananga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa
Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida, Makamu Mwenyekiti Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama na viongozi wengine
wa Chama na Serikali. |
|
Naibu Waziri Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor
Mbarouk (kushoto) akiagana na Naibu Waziri Mambo ya Nje Ethiopia Mhe. Balozi Birtukan
Anayo baada ya kukamilika kwa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Ethiopia katika
mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma baada ya kuweka jiwe hilo huku
wakishuhudiwa na Balozi wa
Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.