Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Kiyoto Tsuji walipokutana katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Kiyoto Tsuji (hayupo katika picha) walipokutana katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
|
kikao kikiendelea
|
kikao kikiendelea |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Kiyoto Tsuji katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao katika mazungumzo yao wamekubaliana kuendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Waziri Makamba ameishukuru Serikali ya Japan kwa kuendelea kuwa mdau mzuri wa maendeleo kwa Tanzania ambapo imekuwa ikiipatia Tanzania misaada mbalimbali ambayo imekuwa mchango chanya kwenye maisha ya Watanzania wengi na hivyo kusaidia jitihada za Serikali kufikia maendeleo makubwa ya kiuchumi na kuhakikisha maisha bora kwa wananchi wake.
Ametaja misaada ambayo Tanzania inapokea kama misaada kutoka Serikali ya Japan kuwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa, barabara ya mzunguko ya Dodoma, barabara ya Holili Arusha na Soko la Malindi Zanzibar kuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo Tanzania imenufaika nayo kupitia uhusiano na ushirikiano na Japan.
“Nitumie nafasi hii kuishukuru Serikali ya Japan kwa kukubali kwake mradi wa Upanuzi wa bandari ya Kigoma ambao utaiunganisha Tanzania na Mashariki mwa nchi ya DRC pamoja na Zambia na Burundi ambazo pia ni watumiaji wa Ziwa Tanganyika,” alisema Mhe. Waziri.
Amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha inaongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kati yake na Japan na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kwa manufaa ya pande zote mbili.
Amesema Tanzania na Japan zimekuwa zinashirikiana kupitia maeneo ya elimu kwa kusaidia kujenga uwezo kwa Watanzania, afya, miundombinu, nishati jadidifu Diplomasia na ushirikiano wa kimataifa.
Naye Mhe. Tsuji ameeleza
utayari wa Japan kuendelea kushirikiana na Tanzania
kuimarisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Japan.
Ameipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika masuala ya amani duniani kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa na nchi nyingine na hivyo kutoa mchango mkubwa kwa uwepo wa amani na usalama duniani.
Amesema Japan iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuongeza biashara na bara la Afrika na kushirikiana kukuza ushirikiano na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kwa manufaa ya pande zote mbili.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.