Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) ameeleza
kuwa msisitizo wa Sera ya Mambo ya Nje ni Diplomasia ya Uchumi wakati
akiwasilisha makadirio ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara tarehe 28
Mei, 2024 bungeni jijini Dodoma.
Katika hotuba hiyo amelifahamisha Bunge kuwa, Wizara imekamilisha rasimu ya awali ya Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi itakayotoa mwongozo wa utekelezaji wa majukumu yake.
”Mkakati huo umeainisha maeneo saba ya kipaumbele ambayo Wizara itayatilia mkazo katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi”, Alisema Waziri Makamba.
Maeneo hayo ni pamoja na; kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi, kuvutia watalii kuja Tanzania, kutafuta misaada na mikopo ya masharti nafuu kutoka nje, kutafuta fursa za ajira na masomo kwa Watanzania nje ya nchi, kujenga taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa, kujenga wezo wa kitaasisi wa Wizara, na Wizara na Taasisi nyingine kusimamia vizuri utekelezaji wa Mkakati wa Diplomasia ya Uchumi.
Aidha, kukamilika kwa mkakati huo kutaiwezesha Serikali na wadau wote kutambua majukumu yao katika mnyororo wa hatua za kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa.
Utekelezaji wa diplomasia ya uchumi umeiwezesha nchi kuingia makubaliano mbalimbali yenye tija kwa Taifa. Makubaliano hayo yamewezesha kupata mikopo nafuu na misaada, kuvutia watalii, kupata masoko ya bidhaa zetu, kuvutia wawekezaji na wabia wa aina mbalimbali wa maendeleo yetu.
Mafanikio mengine yaliyopatikana ni; kupata masoko ya bidhaa na huduma nje ya nchi, kuwezesha uagizaji bidhaa na huduma muhimu kutoka nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya ndani; na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje.
Wizara imefanikisha jukumu hilo kwa kushirikiana na Wizara za kisekta, Taasisi za Umma na Sekta Binafsi ambapo zimekuwa zikiratibu makongamano mbalimbali ya biashara na uwekezaji yanayofanyika pamoja na ziara za Mheshimiwa Rais nchi za nje. Vilevile, kuratibu ziara za watendaji wa serikali katika nchi na kuzungumzia masuala ya kiuchumi, biashara na uwekezaji kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.

No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.