Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amewasili jijini Paris, Ufaransa na kupokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Ali Mwadini tarehe 12 Mei, 2024.
Mhe. Makamba anatarajia kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Nishati Safi ya Kupikia barani Afrika utakaofanyika tarehe 14 Mei, 2024 katika Makao Makuu ya UNESCO.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo utaongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye atakuwa Mwenyekiti Mwenza kufuatia mwaliko wa Taasisi ya Kimataifa ya Nishati (International Energy Agency). Aidha, Mhe. Rais anatarajia kuhutubia hafla ya ufunguzi ya Mkutano husika.
Wenyeviti wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Nishati, Dkt. Fatih Birol; Waziri Mkuu wa Norway, Mhe. Jonas Gahr Støre na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina.
Mheshimiwa Waziri Makamba akiwasili jijini Paris, Ufaransa kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia barani Afrika utakaofanyika tarehe 14 Mei, 2024. |
Mhe. Waziri Makamba akizungumza na Mhe. Balozi Mwadini baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa. |
Mapokezi ya Mheshimiwa Waziri January Makamba jijini Paris, Ufaransa. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.