Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Mhe. Murray McCully amewasili
nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 21- 22 Julai, 2013.
Wakati wa ziara hiyo,
Mhe. McCully atafanya mazungumzo na Viongozi wa Kitaifa wa Serikali akiwemo Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb); Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb); Wazri wa Nishati
na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (Mb); na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt.
William Mgimwa (Mb).
Mazungumzo yao yanatarajiwa kujikita katika kuimarisha maeneo
ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na New Zealand. Tanzania ina lenga kujifunza
kutoka New Zealand kutokana na nchi hiyo kupata mafanikio makubwa katika sekta ya
kilimo hususan ufugaji na viwanda vya kusindika maziwa na mazao mengine.
Eneo lingine ambalo Tanzania inataka kushirikiana na New
Zealand ni sekta ya nishati mbadala. Tanzania imedhamiria kukarabisha makampuni
ya New Zealand kuwekeza nchini katika uzalishaji wa nishati ya nguvu ya jua na geothermal.
Kukaribishwa kwa makampuni hayo ni moja ya mikakati ya Serikali
ya kufikia lengo lake la kuwapatia umeme asilimia 30 ya wananchi wa vijijini ifikapo
mwaka 2015.