Thursday, August 29, 2013

MAAZIMIO YA BARAZA LA KATIBA LA WIZARA




TAARIFA KWA UMMA



MAAZIMIO YA BARAZA LA KATIBA LA 

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA

USHIRIKIANO WA KIMATAIFA


Baraza la Katiba la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa lilikutana tarehe 26 Agosti, 2013 kujadili Rasimu ya Katiba mpya.  Mkutano huo ulifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Mkutano ulifanyika chini ya Uenyekiti wa Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kufunguliwa na mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Balozi wa Tanzania nchini Misri na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mabalozi Wastaafu, Wafanyakazi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.
  
Wizara iliamua kuunda Baraza la Katiba kwa kuzingatia kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ni Wizara ya Muungano; Rasimu ya Katiba imependekeza masuala ya Sera ya Nje kuendelea kuwa miongoni mwa masuala ya Muungano; na kuwa yako masuala yaliyopendekezwa kwenye rasimu ya Katiba ikiwemo mipaka, uraia na muundo wa muungano ambayo yanagusa majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Baraza la Katiba la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, liliazimia mapendekezo yafuatayo katika maeneo ya Mipaka, Muundo wa Jamhuri, Uraia wa Jamhuri na Sera ya Mambo ya Nje:- 

1)             Mipaka ya nchi iwekwe wazi mwishoni mwa Ibara ya 2 ili isomeke kama ifuatavyo: “Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na Zanzibar ikijumuisha ardhi, maziwa na sehemu yake ya bahari (Territorial Waters) pamoja na anga kwa mujibu wa sheria za kimataifa;

2)             Baraza pia lilipendekeza mabadiliko katika Muundo wa Jamhuri ya Muungano kwamba Muundo wa Serikali Mbili uliopo, uendelee na kuboreshwa kwa kuwekewa mifumo imara ya kisheria itakayoakisi maslahi ya pande zote mbili za Muungano ili kupunguza changamoto na manung’uniko kutoka kwa wadau wa Muungano. 

3)             Kuhusu suala la uraia katika Jamhuri ya Muungano; Baraza lilipendekeza kuwa suala la uraia wa nchi mbili kwa Mtanzania wa kuzaliwa litamkwe Kikatiba na Raia huyo asipoteze uraia wake wa kuzaliwa kwa sababu ya kupata uraia wa nchi nyingine. Uraia wa nchi mbili utatoa fursa kwa Taifa letu kufaidika kimaendeleo kutokana na kutumia rasilimali za Watanzania walioko nje ya nchi;

4)             Kuhusu Uraia, Ibara ya 55(4) inayozungumzia kumpa uraia wa kuzaliwa mtoto atakayekutwa ndani ya mipaka ya nchi yetu, ambaye wazazi wake hawajulikani ni raia wa nchi gani,  Baraza linapendekeza “….Uraia huo utasitishwa endapo uraia wa asili (wa nchi nyingine) wa mtoto huyo utagundulika na kuthibitishwa pasipo na shaka au kama itagundulika kuwa ulifanyika udanganyifu wa kumtupa kwa makusudi mtoto huyo kwa nia ya kupata uraia wa Jamhuri ya Muungano.”

5)             Kuhusu Uraia wa kuandikishwa, Ibara ya 56(2), mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muungano anaweza kutuma maombi ya kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano baada ya kuomba uraia wa Muda wa kuishi nchini kama mwanafamilia wa ndoa (dependant) mpaka ndoa iwe imedumu kwa miaka kadhaa (miaka itamkwe na sheria)”.

6)             Kuhusu Sera ya Mambo ya Nje; Baraza linapendekeza mabadiliko katika Ibara ya 12 ya rasimu kwamba Misingi (Principles) ya Sera ya Mambo ya Nje ijumuishwe badala ya majukumu ya Wizara kwa kuwa majukumu hubadilika na nyakati. Aidha, Katiba ilielekeze Bunge litunge Sheria itakayosimamia utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania.

7)             Kuhusu Ibara ya 39 (3) inayohusu raia wa Tanzania kutokupelekwa nje ya nchi kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote bila ya ridhaa yake, Baraza linapendekeza Kifungu hicho kifutwe, kwa sababu kuna ugumu wa haki inayotajwa kwenye Kipengele hiki kutekelezeka bila kuathiri wajibu ya kimataifa wa nchi (international obligations) katika makosa ya jinai, kwa kuwa ni vigumu sana kupata ridhaa ya mtuhumiwa kuhojiwa kwa makosa aliyoyatenda au anayotuhumiwa kuyatenda.


WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

28 AGOSTI, 2013

EU Members of Parliament visit Tanzania


Ambassador Rajabu Gamaha, Acting Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation welcomes Hon. Hannes Swoboda, Member of the European Parliament (MEP) and President of the Social Democrats in the European Parliament.  Hon. Swoboda paid a courtesy visit earlier today to discuss matters of regional integrations, promotion of good governance and accountability, areas of cooperation that include piracy, oil and gas.

Ambassador Gamaha greets H.E. Filberto Cerian Sebregondi, Head of Delegation of the European Union. The EU delegation arrived in Dar es Salaam earlier today from Brussels, Belgium.

Ambassador Gamaha welcomes Hon. Norbert Neuser, Member of the European Parliament (MEP) and Social Democrats Coordinator.

Ambassador Gamaha welcomes Hon. Ricardo Cortes, Member of the European Parliament and Social Democrat Coordinator for Development. 

Ambassador Gamaha explains about the progress of the custom union in the East African Community (EAC) and the success of the free trade area in the Southern Africa Development Community. 

THe European Delegation during the meeting. 

Tanzania delegation that include Ambassador Dora Msechu, Director of the Department of Europe and Americas and Mr. Frank Mhina, Foreign Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. 

The meeting continues.

On a separate meeting, Ambassador Rajabu Gamaha, Acting Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation took time to meet with H.E. Filberto Cerian Sebregondi, Head of Delegation of the European Union.  

Ambassador Gamaha listens to Head of the EU Delegation Filberto Cerian Sebregondi during their meeting. Also in the photo is Ambassador Dora Msechu, Director of the Department of Europe and Americas in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. 



All photos by Tagie Daisy Mwakawago  




TANZIA



Uteuzi wa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria


Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa akutana kwa mazungumzo na Mwenyekiti wa Tume ya Ukaguzi ya Ufilipino


Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimkaribisha Wizarani Bibi Maria Gracia Pulido-Tan, Mwenyekiti wa Tume ya Ukaguzi ya Jamhuri ya Ufilipino alipofika kwa ajili ya mazungumzo. Bibi Pulido-Tan pia ni Mgombea wa Jamhuri ya Ufilipino kwenye Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa. 

Bibi Pulido-Tan akimtambulisha kwa Balozi Mushy,  Bi. Donna Celeste Feliciano-Gatmaytan, Kaimu Balozi wa Ufilipino nchini Kenya.

Balozi Mushy akiwa katika mazungumzo na Bibi Pulido-Tan kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kimataifa.

Baadhi ya wajumbe kutoka Ufilipino waliofuatana na Bibi Pulido-Tan.

Balozi Mushy akiendelea na mazungumzo na Bibi Pulido-Tan huku Bi. Rose Kitandula (kulia), Afisa Mambo ya Nje akinukuu mazungumzo hayo.


Bibi Pulido-Tan akimweleza jambo Balozi Mushy wakati wa mazungumzo yao.

Mazungumzo yakiendelea.

Balozi Mushy katika picha ya pamoja na Bibi Pulido-Tan mara baada ya mazungumzo yao.

Picha ya pamoja.

Tuesday, August 27, 2013

TAARIFA KWA UMMA


Mhe. Waziri Membe akielezea kuhusu suala la uraia wa nchi mbili. 



TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kuujulisha Umma kuwa jana tarehe 26 Agosti, 2013, Mheshimiwa Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alikutana na Uongozi wa Tume ya Marekebisho ya Katiba.  Lengo la kukutana na Tume ilikuwa ni kuwasilisha pendekezo la haki ya Uraia wa nchi mbili kutamkwa na kutambuliwa kwenye Katiba mpya.

Mheshimiwa Waziri alikutana na Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Joseph Sinde Warioba, Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Augustino Ramadhani, Makamu Mwenyekiti wa  Tume pamoja na Katibu wa Tume na Naibu Katibu wa Tume.

Akiwasilisha hoja yake mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba, Mheshimiwa Waziri alisema yafuatayo:-

1.    Suala la Uraia wa Nchi mbili haliko kwenye rasimu ya sasa iliyotolewa.  Lengo la kufika Tume ni ni kuomba suala hilo liingizwe kwenye rasimu.

2.    Amependekeza Katiba itamke kwamba, Raia wa Tanzania aliyeko nje hatafutiwa uraia wake na mtu yeyote, chombo chochote sheria au Katiba, eti tu kwa sababu raia huyo amechukua uraia nje ya nchi.

3.    Katiba ikitamka hivyo, itungwe Sheria itakayofafanua haki, wajibu na masharti ya Mtanzania mwenye uraia wa nchi mbili.

4.    Katika kujenga hoja hizo tatu, Tume ilielezwa faida zitakazopatikana kwa kuitambua na kuishirikisha jamii ya Watanzania waliopo ughaibuni (Diaspora).  Tume pia iliondolewa wasiwasi juu ya madai kuwa uraia wa nchi mbili unahatarisha usalama wa taifa au utawafanya baadhi ya watu kupiga kura wakiwa nje. Tume iliambiwa kuwa Sheria za Uchaguzi hutawala upigaji kura kwa raia walio ndani  na nje na hauwi  holela.  Kuhusu suala la usalama, Waziri alisisitiza kama ni mashaka, basi mashaka hayo yawe kwa wageni wanaoomba uraia  nchini kuliko watanzania walioko nje.


Katika kumalizia, Mheshimiwa Waziri alisisitiza, “bado naamini watanzania walioko nje sio wasaliti, They are just as smart citizen”.



IMETOLEWA NA:


 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA 

KIMATAIFA


27 Agosti, 2013