|
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Rosemary Jairo akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa Habari juu ya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania Diaspora and SMEs partnership 2015) litakalofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015, likiwa na kaulimbiu isemayo 'Creating Linkages between Diaspora and local SMEs in Tanzania' |
|
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea
Picha na Reginald Philip
|
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu:
255-22-2114615, 211906-12
Nukushi:
255-22-2116600
|
|
|
20 KIVUKONI FRONT P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM, Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa (International Trade Centre
UN-Agency) inafanya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania Diaspora & SMEs Partnership Conference 2015). Kongamano
husika litafanyika hapa Dar es Salaam, kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015
katika Hoteli ya Serena. Kongamano hilo litakuwa la pili kufanyika hapa nchini
na litahusisha Diaspora na Wadau wa hapa Tanzania.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Rais na Utawala Bora – Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu ndio Wadau
Wakuu katika Maandalizi ya Kongamano hili.
Kongamano la mwaka huu lina
Kauli Mbiu, ‘Creating Linkages between Diaspora and Local SMEs in Tanzania’
na Dhumuni lake ni kuhamasisha Ushiriki wa Diaspora katika kukuza Biashara
Ndogo na za Kati hapa nchini. Kongamano la mwaka huu pia litahusisha Mikoa ya
Tanzania ambapo Mikoa itapata fursa ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo
Mikoani.
Kongamano hilo linatarajiwa kufunguliwa na Mhe.
Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa na
Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi.
Aidha,
katika kuhitimisha kilele cha Kongamano hilo, Diaspora wanatarajiwa kufanya
ziara Zanzibar tarehe 15 Agosti 2015, ikiwa ni sehemu ya mwaliko maalum kutoka
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Pamoja na Shughuli za Ufunguzi na Kilele, Matukio
muhimu yatakuwa ni Maonesho ya Kibiashara, Majadiliano ya Mada kuhusu
Ushirikishwaji wa Diaspora kwa Maendeleo ya Nchi hususan SMEs, uwekezaji
Mikoani n.k.
Kongamano hilo litahudhuriwa
na Watanzania Wanaoishi Ughaibuni (Diaspora) na wale waliorejea hapa nchini na
Wadau wa Maendeleo kutoka hapa nchini.
Wizara ya Mambo ya Nje Usually integration involves one or more written agreements that
describe the areas of cooperation in detail, as well as some coordinating
bodies representing the countries involved.inawakaribisha kushiriki nasi katika Kongamano
hilo. Tafadhali tembeleeni tovuti ya (www.tzdiaspora.com) kupata taarifa muhimu
hususan kuhusu Ada za Ushiriki, fursa za Kufadhili na namna ya kujisajili.
Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Dar es Salaam
21 Julai, 2015