Tuesday, October 27, 2015

Jukwaa la Vijana wa ICGLR watembelea Wizara ya Mambo ya Nje

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na wawakilishi kutoka Jukwaa la Vijana la Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa  Maziwa Makuu (ICGLR Youth Forum) (hawapo pichani) walipofika Wizarani kwa lengo la kumsalimia na kumpongeza kwa kuteuliwa katika nafasi ya Katibu Mkuu. Timu  hiyo ya vijana  kutoka nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu ipo nchini kama Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania. Wengine katika picha ni Balozi Muburi Muita, Mkuu wa Msafara na Mratibu wa Kitaifa wa ICGLR nchini Kenya pamoja na Bi. Nancy Kaizilege.
Sehemu ya Vijana hao wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani). Vijana hao wanatoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Angola, Zambia, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania na DRC.
Balozi Muburi nae akizungumza wakati wa mkutano kati ya Wawakilishi wa Jukwaa la Vjana wa ICGLR na Balozi Mulamula.
Sehemu nyingine ya vijana wakifuatilia mkutano wao na Balozi Mulamula (hayupo pichani)
Bi. Nancy nae akitoa maelezo mafupi kuhusu dhumuni la ziara ya Vijana hao hapa Wizarani.
Vijana wakifuatilia

Picha ya pamoja. 



Mkataba wa Makubaliano kuhusu Misaada ya Kibinadamu kwa Wakimbizi huko Kigoma wasainiwa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa pamoja na Bw. Anton Breve, Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Madaktari wasio na Mipaka wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu Misaada ya Kibinadamu kwa Wakimbizi waliopo Kigoma. Uwekaji saini huo umefanyika Wizarani tarehe 27 Oktoba, 2015.
Balozi Mulamula na Bw. Breve wakibadilishana Mkataba huo wa Makubaliano mara baada ya kusainiwa
Balozi Mulamula akiwa kwenye mazungumzo na Bw. Breve kabla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu Misaada ya Kibinadamu kwa Wakimbizi waliopo Mkoani Kigom.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Baraka Luvanda (kushoto)  kwa pamoja na Maafisa katika Kitengo hicho Bw. Gerald Mbwafu (katikati) na Bw. Elisha Suku (kulia) wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Bw. Breve (hawapo pichani). 

Monday, October 26, 2015

Balozi Mwakasege awasilisha Hati za Utambulisho nchini Malawi

Tarehe 22 Oktoba, 2015 Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege alipata fursa ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika katika Ikulu ya Kamuzu Palace mjini Lilongwe.
Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akipigiwa nyimbo za taifa za Malawi na Tanzania huku akishuhudiwa na maafisa Ubalozi.
Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Kamuzu Palace mjini Lilongwe. Wanaoshuhudia ni maafisa Ubalozi Wilbroad A. Kayombo kushoto, Elyneema Lissu, Nimpha Marunda na Mbonile Mwakatundu
Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Prof. Arthur Peter Mutharika
Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akiagana na Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika 
Watumishi wa Ubalozi wakiwa na Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege nyumbani kwake

Friday, October 23, 2015

Mabalozi wa Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wamtembelea Katibu Mkuu Nje.

Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe. Filiberto Sebregondi akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.
Ujumbe ulioambatana na Balozi Sebregondi, wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Joseph Sokoine (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Balozi Samwel Shelukindo, wakifuatilia mazungumzo hayo. 
 Ujumbe ulioambatana na Balozi Sebregondi, wakifuatilia mazungumzo hayo.
 Mkutano ukiendelea.
===============
PICHA NA: REUBEN MCHOME.

Balozi Luvanda akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uturuki

Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Baraka Luvanda akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Yasemin Eralp. Mazungumzo hayo yalihusu ukimalishaji wa Makubaliano mbalimbali kati ya Tanzania na Uturuki ili yaweze kusainiwa na kuanza kutekelezwa.
Balozi Luvanda akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Yasemin Eralp akimsikiliza kwa makini Balozi Luvanda ambaye hayupo pichani
Balozi wa Uturuki akibadilishana mawazo na Afisa wake wakati wa mazungumzo hayo
Balozi wa Uturuki, Mhe. Yasemin Eralp akimkabidhi nyaraka Balozi Luvanda
Balozi Luvanda pamoja na Afisa wake, Bw. John Pangipita wakimsikiliza Balozi wa Uturuki hayupo pichani.

Mazungumzo yanaendelea





Tanzania na Malawi zawasilisha Rasimu ya Azimio kuhusu Watu wenye Ualbino

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa  Balozi Tuvako Manongi akifurahia jambo na Bi Ikponwosa Ero mwenye Ualibino mara  baada ya mazungumzo yao  ambapo walibadilisha mawazo kuhusu pamoja na mambo mengine,   changamoto zinazowakabili watu wenye ualibino na namna gani jumuiya ya kimatifa inaweza kushirikiana katika kuzikabili changamoto hizo. Bi Ikponwosa  aliteuliwa mwezi Agosti Mwaka huu na  Kamisheni ya  Haki za Binadamu  ya Umoja wa Mataifa kama  Mtaalamu huru anayeendesha kampeni,  uhamasishaji, uelimishaji  na  uwezeshaji kuhusu watu wenye ualibino na changamoto  zinazowakabili  watu wenye ualibino. Bi Ero ni   Mzaliwa wa Nigeria mwenye uraia wa Canada.
 
Na  Mwandishi Maalum, New York

Kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ualibino, Wakilishi za Kudumu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Malawi katika Umoja wa Mataifa, zimewasilisha rasimu ya azimo kuhusu watu wenye ualibino.

Rasimu ya azimio hilo inalenga katika kuzishawishi na kuzitaka Jumuiya ya Kimataifa kuendelea na juhudi za kutetea haki na ustawi wa watu wenye ualibino ikiwa ni pamoja na kuliwanda.

Azimio hilo limewasilishwa kupitia Kamati ya Tatu ya Utamaduni,  Haki za Binadamu na Jamii ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,  na ambalo limekwisha kusambazwa kwa nchi wanachama na wadau wengine kwa ajili ya kupata maoni na kuungwa mkono.

Azimio hilo linajielekeza pia katika kusisitiza upatikanaji wa fursa za elimu, huduma za afya na ajira kwa watu wenye ualibino, maeneo ambayo ni changamoto kubwa kwa watu hao.

Kupitia azimio hilo, Tanzania na Malawi,  zinaitaka Jukumuiya ya Kimataifa kuunga  mkono jitihada zinazofanywa na nchi ambazo tayari zimejiwekea sera, sheria na mipango ya pamoja na  mambo mengine, kuwalinda watu wenye ualbino na kuwapatia fursa mbalimbali za maendeleo kama raia wengine.

Vile vile, azimio hilo linamwomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  kuwasilisha taarifa kuhusu hali za watu wenye ualibino mkazo ukiwa katika changamoto wanazokabiliana nazo,  na juhudi ambazo zimechukuliwa na nchi wanachama katika kuzikabili.

Taarifa hiyo ya Katibu Mkuu inaombwa kuwasilishwa wakati wa Mkutano wa  71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa chini ya ajenda ya Maendeleo ya Jamii.

Azimio hilo pia linasisitiza haja na umuhimu wa kutambua juhudi zinazofanywa katika ngazi ya nchi na Ki- Kanda, na hivyo Katibu Mkuu anaombwa kuwasilisha katika Baraza Kuu la 71 la Umoja wa Mataifa,  mapendekezo ya namna ya kuimarisha uwezo na juhudi za nchi husika katika kulitafutia ufumbuzi tatizo la  watu wenye ualibino kwa kadri nchi hizo zitakavyoomba.

Katika sehemu ya utangulizi wa Azimio, Azimio linatambua juhudi mbalimbali na taarifa za vyombo vingine kama Vile Baraza la Haki za Binadamu, Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu haki za watu ,kuzuia vitendo viovu na ubaguzi dhidi ya watu wenye ualbino.

Azimio linaeleza hofu dhidi ya uovu wanaofanyiwa watu wenye ualibino wakiwamo wanawake na watoto.

Thursday, October 22, 2015

Taarifa kwa Vyonbo vya Habari


Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki au kujeruhiwa huko Saudi Arabia

Mahujaji wengine wawili kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki  dunia. Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini na saba (27). Majina kamili ya mahujaji hao ni Bw. Juma Yussuf Bakula na Bw. Ahmad Awadh Namongo kutoka Kikundi cha Ahlu Dawaa.
Hadi sasa mahujaji kumi na tatu (13) kutoka Tanzania bado hawajulikani walipo na jitihada za kuwatafuta bado zinaendelea.

Kwa upande wa mahujaji wanne ambao walikuwa wanapatiwa matibabu kutokana na kuugua au kujeruhiwa, mmoja wao ni Bw. Mustafa Ali Mchina ambaye alikuwa amelezwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika mji wa Maddinah alifariki dunia tarehe 17 Oktoba 2015 na kuzikwa Maddinah siku hiyo hiyo. Bi. Mahjabin Taslim Khan ambaye alijeruhiwa katika ajali hiyo na kusababisha kukatwa mguu wake amepata nafuu na alirejea nchini tarehe 20 Oktoba 2015. Mwingine ni Bi. Hidaya Mchomvu ambaye alijeruhiwa pia bado yupo hospitali akiendelea kupatiwa matibabu. Hujaji wanne ni Bw. Ahmed Abdallah Jusab ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo alifanyiwa upasuaji wa kumuwekea kifaa cha kuongeza mapigo ya moyo tarehe 19 Oktoba 2015 na alitarajiwa kurejea nchini tarehe 21 Oktoba 2015.
 
Serikali ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za kuwatambua mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
22 Oktoba, 2015

Waziri Membe aagana na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akifungua hafla ya kumuaga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe iliyoandaliwa na watumishi wa Wizara hiyo na kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa waliohudhuria hafla hiyo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akitoa muhtsari wa shughuli chache ambazo Waziri Membe alizisimamia kwa umahiri mkubwa katika kipindi chake cha miaka 9 ya Uwazi wa Mambo ya Nje. Waliokaa ni Mhe. Membe na Balozi Mulamula ambao wanasikiliza kwa maikini shughuli zilizotekelezwa na Mhe. Waziri Membe.

Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakisikiliza kwa makini shughuli ambazo Mhe. Waziri Membe amezisimamia ipasavyo ikiwemo suala la maslahi ya watumishi.

Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakisikiliza kwa makini shughuli ambazo Mhe. Waziri Membe amezisimamia ipasavyo ikiwemo suala la maslahi ya watumishi

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akitangaza Tuzo na Zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa kwa ajili ya Mhe. Waziri na Naibu Waziri na Wenza wao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kushoto) akisoma maneno yaliyoandikwa katika Tuzo ya Uongozi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na kukabidhiwa na Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula 

Waziri Membe akifurahia zawadi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje.

Waziri Membe akipokea zawadi kwa niaba ya Mama Membe ambaye hakuweza kufika katika hafla hiyo. Bi. Amisa Mwakawago, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu alikabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya Wizara.

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Begum Karim Taj naye akikabidhi zawadi kwa Mhe. Waziri kwa niaba ya Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania

Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahya akipokea zawadi kwa niaba ya Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim ambaye hakuweza kuhudhuria hafla hiyo kutokana na majukumu ya kitaifa.

Balozi Mulamula na Mama Mwakawago wakionesha zawadi ya Mama Mahadhi Juma Maalim.
Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wakishuhudia zoezi la utoaji wa zawadi.

Waziri Membe akiongea na watumishi wa Wizara wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Itifaki, Balozi Juma Maharage akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy naye akiongea machache katika hafla hiyo

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Elibariki Maleko akionekana mtu mwenye furaha katika hafla hiyo, baada ya kutangazwa kuwa ameteuliwa kuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uganda. Wengine waliotangazwa kuwa Naibu Mabalozi ni Bi. Rosemary Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora ambaye anakuwa Naibu Balozi nchini Afrika Kusini na Bw. Andy Mwandembwa, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Itifaki ambaye anakuwa Naibu Balozi nchini Sweden.

Wakati wa maakuli. Mhe. Waziri akiwa ameshikilia sahani ya chakula na anyemfuatia ni Katibu Mkuu anayeonekana akichota chakula

Naibu Katibu Mkuu naye anajichotea chakula

Waheshimiwa Mabalozi nao wanajichotea chakula

Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Idara/Vitengo

Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara/Vitengo.

Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wasaidizi wa Waziri na Naibu Waziri.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
Mhe. Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi Wanawake.