Wednesday, November 25, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje yashiriki maadhimisho ya miaka 45 ya Taifa la Oman



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akitoa hotuba wakati wa Maadhimisho ya miaka 45 ya Taifa la Oman yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Oman hapa nchini na kufanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) tarehe 24 Novemba, 2015. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Salim Ahmed Salim. Katika hotuba yake Balozi Yahya alisifu uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Oman na kuitakia heri nchi hiyo katika kuadhimisha miaka 45.
Balozi wa Oman hapa nchini, Mhe. Soud Al Mohammed Al-Ruqaish akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 45 ya Taifa la Oman. Pia alisifu ushirikiano kati ya Tanzania na nchi yake na kuahidi kuuendeleza na kuuimarisha.
Mhe. Mwinyi (wa kwanza kushoto)  kwa pamoja na Mhe. Salim (wa pili kushoto) na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf (wa pili kulia) wakiwa kwenye sherehe hizo pamoja na wageni wengine waalikwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (kulia) akiwa na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Tahir Khamis (mwenye suti ya kijivu) pamoja na wageni mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya Miaka 45 ya Taifa la Oman.
Kiongozi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Balozi Juma Halfan Mpango (kushoto mwenye suti ya kijivu) akiwa na Balozi wa Burundi hapa nchini, Mhe. Issa Ntambuka wakati wa maadhimisho ya sherehe ya miaka 45 ya Taifa la Oman.
Balozi wa Oman, Mhe. Al-Ruqaish akiwaongoza Viongozi Wastaafu, Mabalozi na Mgeni rasmi Balozi Yahya kukata keki kama ishara ya kusherehekea siku hiyo kubwa kwa Taifa la Oman.
Wageni waalikwa wakifuatilia sherehe hizo akiwemo Afisa Mambo ya Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Batholomeo Jungu (mwenye suti ya kijivu)
Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia sherehe za miaka 45 ya Taifa la Oman. Kutoka kulia ni Bw. Ali Ubwa, Bw. Seif Kamtunda na Bw. Hangi Mgaka.
Mhe. Mwinyi akijadili jambo na Mhe. Salim kabla ya kuanza kwa sherehe hizo za miaka 45 ya Taifa la Oman
Picha ya Juu na Chini ni Sehemu ya Wageni waalikwa wakati wa sherehe za miaka 45 ya Taifa la Oman

Sehemu nyingine ya Wageni waalikwa

Wageni waalikwa






Balozi Mushy amuaga Mwakilishi wa UNICEF nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini Dkt. Jama Gulaid aliyemaliza muda wake wa Uwakilishi nchini.
Moja ya zawadi alizopokea kutoka kwa Balozi Mushy ni Kitabu kinachoelezea Vivutio mbalimbali vya Utalii vinavyo patikana hapa nchin.

Pia katika mazungumzo yao, Balozi Mushy alimpongeza Dkt. Gulaid kwa kuiwakilisha vyema   UNICEF hapa nchini. kwa Upande wa Dkt. Gulaid naye alitumia fursa ya kumshukuru Balozi Mushy kwa niaba ya Wizara  na Serikali kwa ujumla kwa Ushirikiano mkubwa alioupata katika kipindi chote cha uwakilishi wa UNICEF hapa nchini.   
Balozi Mushy akizungumza na Dkt. Gulaid
Dkt. Gulaid naye akizungumza huku Balozi Mushy akimsikiliza.


Picha na Reginald Philip

Tuesday, November 24, 2015

Balozi Mushy akutana na Mjumbe Maalumu kutoka Poland



Juu na Chini Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akifanya mazungumzo na Mjumbe maalumu kutoka Poland Balozi Anna Gropinska, alipomtembelea Wizarani mapema leo tarehe 24 Novemba 2015 jijini Dar es Salaam



Algeria Embassy Celebrates National Day

Acting Permanent Secretary at the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Amb. Celestine Mushy who was the Guest of Honor at the Algeria's National Day Reception delivers a speech on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania. The reception held at the New Africa Hotel on Friday 20th 2015.
Ambassador of Algeria to Tanzania, H.E Saad Belabed delivers a speech at that Algeria's National Day Reception.
Invited guests who were diplomatic community in the country and officials from various public and private institutions listen the speeches.
Acting Permanent Secretary at the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Amb. Celestine Mushy (L) and
Ambassador of Algeria to Tanzania, H.E Saad Belabed raise their glasses in a toast to the 61 anniversary of Algeria Independence.

Director of Africa Department at the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Amb. Samuel Shelukindo (R) exchanges views with the Algeria Ambassador prior the beginning of the reception.

Acting Permanent Secretary at the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Amb. Celestine Mushy (L) is greeting people when he was arriving at the reception hall.

A group photo, from left is Amb. Mushy, Ms. Halima Abdallah, H.E Belabed and Amb. Shelukindo.

Monday, November 23, 2015

TANZANIA PUBLIC SERVICE PENSIONS FUND RECEIVES THE GOLDEN AWARD FOR QUALITY AND BUSINESS PRESTIGE IN GENEVA, SWITZERLAND

The award was received on behalf of PSPF by Ambassador Modest J. Mero, Permanent Representative of Tanzania to UN, at the ceremony held at Hotel Intercontinental in Geneva on 23 November 2015. 
The PSPF has received the Golden award for Quality and Business Prestige from the Association Otherways Management and Consulting based in Paris, France in recognition of her achievements in areas of Innovation, Quality Commitment and Excellence.

Friday, November 20, 2015

Safari ya Mwisho ya Marehemu Bi. Nyami Ivan Lusinde, Dodoma Tanzania


Ndugu wa Marehemu Bi. Nyamiti Ivan Lusinde wakiwa mbele ya Jeneza alilo hifadhiwa marehemu wakiwa na huzuni wakati wa ibada ya kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele, Mama mzazi wa  marehemu, Mama Agness Lusinde na katikati ni Ndugu wa Marehemu Bw. Malima Lusinde
Mahala alipozikwa Marehemu Bi. Nyami Ivan Lusinde


Wednesday, November 18, 2015

New IOM Chief to Tanzania Presents Letter of Credence

Permanent Secretary at the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Amb. Liberata Mulamula (R) receives letters of Credence from New Chief of Mission of International Organization for Migration (IOM) to Tanzania, Dr. Qasim Sufi. Dr. Sufi is coming from Chad where he was holding the same position.
New IOM Chief of Mission to Tanzania (L) is in official talks with Amb. Mulamula, that focussed on the importance of strengthing cooperation between IOM and Tanzania. Amb. Mulamula thanked IOM for their various aids extended to Tanzania including the formulation of Diaspora web portal that is to be inaugurated on 30th of this month.
Ofiicials from Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation. Left is the Director of Diaspora, Amb. Anisa Mbega and Ms. Tagie Mwakawago.

The official talks.


Group photo
Mr. Sufi says goodbye to the Permanent Secretary after letter of Credence presentation execise is completed.

Rais Magufuli asaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa, awasili Mjini Dodoma kwa Gari

Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo
katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya Watu zaidi ya 120 vilivyotokana
na mashambulizi ya kigaidi jijini Paris majuzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mama Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na
mashambulizi ya kigaidi  majuzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph  Magufuli akizungumza na
Balozi wa Ufaransa nchini Mama Malika Berak mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mhe.  Francois Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 120 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya
pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
 
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili mkoani Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Mhe. Chiku Galawa. Rais Magufuli amesafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa kutumia usafiri wa Gari.

Tuesday, November 17, 2015

Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na wageni mbalimbali waliotembelea Wizarani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa Serikali ya China katika masuala ya Afrika, Balozi Zhong Jianhua alipotembelea Wizarani tarehe 17 Novemba, 2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Samuel Shelukindo kwa pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Zhong Jianhua (hawapo pichani)
Maafisa waliofuatana na Balozi Zhong Jianhua (hayupo pichani) nao wakifuatilia mazungumzo
Mazungumzo yakiendela



...Mkutano wa Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari 


Balozi Mulamula (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari, Bi. Felistas Mushi alipofika Wizarani kwa mazungumzo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy kwa pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng'itu wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Bi. Mushi (hawapo pichani)


Balozi Mulamula akiagana na Bi. Mushi baada ya mazungumzo yao


Picha na Reginald Philip