Thursday, January 21, 2016

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje akutana na Kaimu Balozi wa Nigeria nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa (kulia) akizungumza na Kaimu Balozi wa Nigeria hapa nchini, Mhe. Salisu Umaru baada ya Balozi huyo kumtembelea Ofisini kwake kwa mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Mazungumzo yakiendelea huku Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, Pamoja na Afisa wa Wizara hiyo Bw. Elisha Suku wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.

Naibu Katibu Mkuu akifurahia jambo na Kaimu Balozi wa Nigeria hapa nchini wakati wa mazungumzo yao.
 Naibu Katibu Mkuu, Balozi Muombwa na Kaimu Balozi Umaru wakibadilishana kadi za mawasiliano  baada ya mazungumzo yao.
===================
PICHA NA REUBEN MCHOME

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimetiliana saini mkataba wa makubaliano wa mashirikiano na Chuo Kikuu cha Komoro

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimetiliana saini mkataba wa makubaliano juu ya mashirikiano na Chuo Kikuu cha Komoro mjini Moroni katika hafla maalum iliyofanyika tarehe 19 Januari, 2016 na kuhudhuriwa na uongozi wote wa Chuo Kikuu cha Komoro, Balozi wa Komoro nchini Tanzania Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Komoro, Bw Mudrik Ramadhan Soragha. 

 Makubaliano kati ya vyuo hivi ni moja ya matokeo ya ziara ya nchini Komoro ya Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoifanya hivi karibuni.

Wednesday, January 20, 2016

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES FOR TANZANIANS IN THE DIASPORA




PRESS RELEASE

PRESS RELEASE
NO BAN ON MINISKIRTS BY PRESIDENT MAGUFULI
The Ministry of Foreign Affairs, East African, Regional and International Cooperation of the United Republic of Tanzania has noticed, with serious concern and disapproval, a grossly distorted report in the Kenyan Standard newspaper, purporting that H.E. President John Pombe Magufuli has banned the wearing of miniskirts in Tanzania.
Unfortunately, the false report, appearing in the daily newspaper's 'MondayBlues' gossip page on 18th January 2016, was taken for factual and circulated widely by other outlets and the social media in Kenya and beyond.The ministry deplores the casual manner in which the Standard handled the hearsay report and the reckless, totally unwarranted attribution of the imaginary 'ban' to the Tanzania Head of State.
While it appreciates the enthusiastic, positive reviews of H.E. President Magufuli's performance in the Kenyan and international media, the Ministry of Foreign Affairs takes strong exception at irresponsible distortions and misreporting, such as the one on miniskirts.
There is no doubt that H.E. President Magufuli and his government are strong proponents of decent dressing, but the ministry wishes to put the record straight that the President has not issued any ban on miniskirts for any reason.
The ministry understands that as a mainstream newspaper, the Standard is obliged to observe the highest standards of journalism, central of which is respect for facts and accurate reporting.
The ministry trusts that the distortion in question was inadvertent, not a malicious attempt to undermine the new administration in Tanzania, and that the Standard will show good faith by at least retracting the wrong information fed to its readers.
-Ends-
Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs, East African, Regional and International Cooperation.

Dar es salaam, January 20, 2016


Tuesday, January 19, 2016

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO BOTSWANA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio Botswana baada ya kuhudhuria mkutano wa SADC mjini Gaborone Januari 18, 2016. 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Watanzania waishio Botswana baada ya kuhudhuria mkutano wa SADC mjini Gaborone Januari 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio Botswana baada ya kuhudhuria mkuatano wa SADC mjini Gaborone Januari 18, 2016.

Monday, January 18, 2016

Balozi Mlima akutana na Kaimu Balozi wa China

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Ponary Mlima (kulia) akisalimiana na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Zhang Biao wakati wawili hao walipokutana kwa ajili ya kufanya mazungumzo Ofisini kwa Katibu Mkuu.
Balozi Mlima akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa China, Mhe. Zhang. Katika mazungumzo hayo, wawili hao waliahidi kuwa nchi zao zitaendelea kushirikiana na kuungana mkono katika masuala mbalimbali ya kimataifa.
Maafisa kutoka Ubalozi wa China uliopo hapa nchini wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Mlima na Mhe. Zhang Biao (hawapo pichani).
Balozi Mlima akimsikiliza Kaimu Balozi wa China, Mhe. Biao
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakinukuu mambo muhimu yaliyojitokeza katika Mazungumzo kati ya Balozi Mlima na Mhe. Biao (hawapo pichani).
Mazungumzo yakiendelea
Picha na Reginald Philip

WAZIRI MKUU, MAJLIWA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO WA SADC GABORONE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Botswana, Bw. Tshenolo Mabeo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama uliopo Gaborone Januari 17, 2016. Majaliwa amemwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa SADC.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mtendaji wa SADC,Dkt, Srergomena Tax mjini Gaborone ambako Mheshimiwa Majaliwa anamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa SADC Januari 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Saturday, January 16, 2016

Waziri Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi wazungumza na waandishi wa Habari

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) akifanunua jambo kwa waandishi wa habari wakati akizungumza na waandishi hao Jijini Dar es Salaam, Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  katika ukumbi mdogo wa mikutano wa  Wizara, Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) alipomtembelea Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (katikati), kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino  ya Serikali wa  Wizara ya Mambo Nje, Bi. Mindi Kasiga.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) alipomtembea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) alipomtembea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Friday, January 15, 2016

Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Reli ya Malaysia

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Ponary Mlima (kulia) akimkaribisha Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya SMH-Rail kutoka Malaysia, Bw. S. Rajamohan, alipokutana nae na kufanya mazungumzo yaliyojikita katika uwekezaji katika sekta ya uchukuzi.
Bw. Rajamohan (kushoto) akizungumza huku Balozi  Mlima akimsikiliza
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (Kushoto) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Khatibu Makenga nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Mlima na Bw. Rajamohan (hawapo pichani).

Picha na Reginald Philip


Waziri Mahiga mgeni rasmi Mahafali ya 18 ya Chuo cha Diplomasia

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), ambaye pia alikua mgeni rasmi wa Mahafali ya Kumi na Nane ya Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam, akifungua rasmi Mahafali hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Kurasini Jijini Dar es Salaam, tarehe 13 Januari, 2016.
Mgeni rasmi Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya chuo hicho, Balozi Mwanaidi Maajar wakiwaongoza wahitimu kuingia katika viwanja vya mahafali.

Mkurugenzi wa Chuo hicho, Dkt. Mohamed Maundi akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mahafali hayo.

Dkt. Watengere Kitojo, Mkurugenzi wa masomo chuoni hapo, akitoa neno la nasaha katika mahafali hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Baraka Luvand wakiwa na wageni wengine waalikwa waliohudhuria mahafali hayo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana (aliyevua kofia), Bw. Lucas Mayenga wote kutoka Wizara ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa  wakiwa ni miongoni mwa wahitimu.
Mgeni Rasmi wa Mahafali hayo, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (katikati), akiwatunuku wahitimu.
Baadhi ya wahitimu wakitunukiwa.

Baadhi ya wahitimu wakifurahia baada ya kutunukiwa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (mbele kushoto), Msaidizi wa Waziri, Bw.Thobias Makoba (wa pili kutoka mbele), Msaidizi wa Naibu Waziri, Bw. Adam Isara, wakifuatilia Mahafali hayo.
Mhitimu Bw. James Bwana ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, akipongezwa na mgeni rasmi, baada ya kutangazwa kuwa Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo katika darasa lake.
Mke wa aliyekuwa Makamu wa Rais Awamu ya Nne, Bi. Asha Bilal (aliyevaa joho) naye alikua miongoni mwa wahitimu katika mahafali hayo.
Bendi ya Jeshi la Polisi, ikisherehesha Mahafali hayo.

Mgeni Rasmi wa Mahafali ya kumi na nane ya Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (MB), akikata keki, huku Mwenyekiti wa Bodi ya chuo hicho, Balozi Mwanaidi Maajar(katikati), Mkurugenzi wa Chuo hicho, Dkt. Mohamed Maundi (kushoto) huku Naibu Waziri, Dkt. Susan Kolimba (nyuma mwenye kitenge) wakifuatilia zoezi hilo.
zoezi la ukataji wa keki likiendelea.
Jukwaa kuu wakiongozwa na mgeni rasmi wakiwa wamesimama  kusikiliza wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.
Wahadhiri wa Chuo hicho nao wakiwa wamesimama  huku wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.


 Mgeni rasmi, Mhe. Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na jukwaa kuu na wahitimu mara baada ya Mahafali hayo.
====================================
Picha na Reginald Philip.

Dr. Mahiga bids farewell to two African Ambassadors

Minister for Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Hon. Dr. Augustine Mahiga (R) is in the conversation with the Namibian Ambassador to Tanzania, H.E Japhet Isaack whose tour of duty in the country is over. In their meeting, the two insisted the importance of enhancing bilateral cooperation between Tanzania and Namibia especially economic cooperation in order to increase the volume of trade.

Dr. Mahiga presents a farewell gift to the Namibian Ambassador to Tanzania who completed his tour of duty.
Minister for Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Hon. Dr. Augustine Mahiga (R) is in the conversation with the Sudanese Ambassador to Tanzania, H.E Yassir Mohammed Ali whose tour of duty in the country is over. In their meeting, the two insisted the importance of enhancing bilateral cooperation between Sudan and Tanzania especially economic cooperation in the areas of irrigation, oil and gas and technology.


Sudanese Ambassador to Tanzania presents gift of various publications to Dr. Mahiga.
Dr. Mahiga presents a farewell gift to the Sudanese Ambassador to Tanzania who completed his tour of duty.

Thursday, January 14, 2016

Waziri Mahiga apokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa UNICEF nchini

Mhe. Waziri Mahiga (kulia), akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Bi. Maniza Zaman

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashiriki, Kikanda na  Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.)  akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa ya Kuhudumia Watoto  (UNICEF), Bi. Maniza Zaman alipokuja Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha  Hati za Utambulisho wake kwa Mhe. Waziri Mahiga.
Bi. Maniza Zaman naye akizungumza na Waziri Mahiga kabla ya kukabidhi Hati zake. 
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Bi. Zaman (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Bi. Mindi Kasiga, Bi. Eva Ng'itu, Afisa Mambo ya Nje na Katibu wa Waziri, Bw. Thobias Makoba.
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Bi. Maniza Zaman


Picha na Reginald Philip