Tuesday, October 18, 2016

Kongamano la Vijana kuelekea maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa lafanyika

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) akiwa katika Kongamano la Vijana lililofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa yatakayofanyika tarehe 24 Oktoba, 2016
Sehemu ya wadau walioshiriki kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 Oktoba, 2o16
Vijana wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) katika Kongamano la Vijana kuelekea maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa
 Balozi  Mushy akiwa na Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Jestas Nyamanga ( wa pili kulia) wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa Kongamano la Vijana
 Watoa mada wakati wa kongamano la vijana

Monday, October 17, 2016

Waziri Mahiga akutana kwa mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa UN Ukanda wa Maziwa Makuu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe.Said Djinnit. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Oktoba, 2016
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Omary Mjenga (wa kwanza kushoto), Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Ally Ubwa kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Bw. Djinnit (hawapo pichani)
Mkutano ukiendelea
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Bw.Djinnit mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika wapitisha Mkataba wa Afrika wa Usalama wa Usafiri Baharini na Maendeleo ya Afrika.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika wapitisha Mkataba wa Afrika wa Usalama wa Usafiri Baharini na Maendeleo ya Afrika.

Mkataba wa Afrika wa Usalama wa Usafiri Baharini na Maendeleo (The African Charter on Maritime Security, Safety and Development) umepitishwa katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Afrika (The AU Extraordinary Summit) uliofanyika tarehe 15 Oktoba, 2016 Lome, Togo. Kupitishwa kwa Mkataba huu kumefuatia makubaliano yaliyofikiwa katika Mikutano ya Kilele ya Wakuu wa Nchi za Afrika iliyofanyika Younde Juni, 2013 na Visiwa vya Shelisheli Februari,2015

Tanzania imewakilishwa katika Mkutano huo na Mhe. Balozi. Dkt. Augustine P. Mahiga (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye hakuweza kuhudhuria Mkutano huu kwa sababu ya Majukumu mengine ya Kitaifa.

Akihutubia Mkutano huo Balozi Dkt. Mahiga alisema, Mkataba huo ni kati ya nyaraka muhimu zitakazoelimisha kuhusu kutunza amani ya Dunia, usalama na maendeleo katika karne hii ya 21. Alisisitiza kwamba Bara la Afrika liko kati ya bahari kuu mbili yaani Atlantic na Hindi ambazo ni kati ya bahari zilizo na shughuli nyingi sana za usafirishaji duniani. Tanzania ikiwa katika nusu ya ukanda wa pwani ya Mashariki na pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi yenye urefu wa Kilomita 1400, Mkataba huu ambao Balozi Mahiga ametia sahihi kwa niaba ya Tanzania ni muhimu sana hivyo amewasihi wanachama wengine kuhakikisha wanafanya hivyo.

Sambamba na hilo Balozi Dkt. Mahiga amesema Mkataba huu si muhimu tu kwa Afrika kulinda bahari na rasilimali zake bali ni muhimu kwa dunia nzima. Balozi. Dkt. Mahiga ameomba Nchi zote na Mashirika ya Kimataifa kuunga mkono utekelezaji wa mkataba huu. Kufuatia kupitishwa kwa mkataba huu ameiomba Sekretariati ya Umoja wa Afrika kupeleka Mkataba huu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na katika Jumuiya ya Kimataifa ili kuweza kutambuliwa.

Aidha, Balozi Mahiga amesisitiza kuwa bahari ni hadhina muhimu si tu ya samaki na gesi bali rasilimali nyinine za thamani kama vile madini ambazo zimekaa tu chini ya bahari hivyo ni jukumu la kila mwana Afrika kuhakikisha analinda rasilimali muhimu tulizo nazo zikiwemo hizi ambazo zinapatikana baharini.

Akimalizia hotuba yake Balozi. Dkt. Mahiga alisisitiza “Hivi karibuni bahari hizi ( Atlantic na Hindi) zitakuwa chanzo muhimu cha nishati, hivyo kusaidia jitihada za kuleta maendeleo kupitia rasilimali za bahari, naamini mkataba huu utakuwa ni silaha muhimu katika kulinda rasilimali hizi za bahari kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo”. Balozi. Dkt. Mahiga ameusihi Umoja wa Afrika na Wanachama wote kuendelea kuuboresha Mkataba huu na kupitisha viambasho muhimu na hatimaye kuharakisha kuuridhia Mkataba huu ili utekelezaji wake uanze bila kuchelewa.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 16 Oktoba, 2016

Ziara ya Mfalme wa Morocco nchini Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ziara ya Mfalme wa Morocco nchini Tanzania

Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini kuanzia tarehe 19 hadi 23 Oktoba, 2016.

Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza zaidi uhusiano kati ya Tanzania na Morocco hususan katika masuala ya kiuchumi na kibiashara kwa faida ya nchi hizi mbili na watu wake.

Vilevile, Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco atatumia fursa ya ziara hiyo kutembelea Zanzibar na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Hata hivyo, ziara hiyo ambayo imejikita zaidi katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara haitaathiri msimamo wa Tanzania katika mgogoro unaoendelea kati ya Morocco na Sahara Magharibi.

Msimamo wa Tanzania ambao umekuwa ukisimamiwa na Awamu zote za uongozi zilizopita na Awamu hii, upo sambasamba na ule wa Umoja wa Afrika (AU) unaoutaka Umoja wa Mataifa (UN) ambao ndio wamepewa jukumu la kusimamia mgogoro huo, kuongeza kasi katika kuutatua na kupata suluhu ya kudumu ya mgogoro huo.

Tarehe 20 Oktoba, 2016 Mhe. Mfalme Mohammed wa VI atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Mhe. Rais Magufuli Ikulu yakifuatiwa na mazungumzo rasmi kati yao na wajumbe waliofuatana nao.

Mhe. Mfalme Mohammed VI pamoja na kutembelea Tanzania, pia atatembelea Rwanda, Ethiopia na Kenya. 

Imetolewa na: 
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dar es Salaam, 
13 Oktoba, 2016.

Thursday, October 13, 2016

Tanzania na China zasaini Mkataba kusaidia sekta za maendeleo nchini

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Charles Mwijage akizungumza katika mkutano kati yake na Naibu wa Viwanda wa Jamhuri  ya Watu wa China, Mhe. Dkt. Qian Keming.Mazungumzo yao yalijikita katika kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na China katika kuboresha miundombinu.
Sehemu ya ujumbe ulioambatana na Dkt. Keming wakimsikiliza kwa makini Dkt. Mwijage hayupo pichani.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Kushirikiana katika masuala ya uchumi na teknolojia
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Ramadhani Muombwa Mwinyi (katikati), na Mwakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania kwa pamoja wakishuhudia uwekwaji saini katika mkataba huo.
Dkt. Mwijage na Dkt. Keming wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkutano.


***********************************************************




Serikali ya Watu wa China imeahidi kuipatia Tanzania msaada wa fedha wa kiasi cha Shilingi bilioni 97 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb) baada ya kukutana na ujumbe kutoka China unaongozwa na Naibu Waziri wa Biashara wa nchi hiyo, Mhe. Dkt. Kian Keming.

Dkt. Kian na ujumbe wake upo nchini ambapo pamoja na mambo mengine walishiriki kikao cha tano cha Kamati ya pamoja ya Uchumi, Biashara, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kiteknolojia kilichofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Mhe. Mwijage alieleza kuwa katika kikao hicho walijadili masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji katika viwanda, miundombinu na nishati. Alisema Serikali ya awamu ya tano imeweka mkazo katika maeneo hayo ili kufikia lengo la nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Alieleza kuwa katika harakati za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2020, viwanda viwili vya chuma na marumaru vilivyojengwa na wawekezaji kutoka China vinatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka ujao. Kiwanda cha tatu kitaanza kujengwa na wawekezaji wa China muda wowote watakapopewa eneo kwa ajili ya ujenzi huo.

Kiwanda cha kwanza ni cha chuma kilichopo Mlandizi mkoani Pwani ambapo kitakapoanza kazi, kitazalisha tani 1,200,000 za chuma kwa mwaka. Aidha, kiwanda kingine cha marumaru kilichopo Mkuranga mkoani Pwani kinatarajiwa kuingiza pato la Dola za Marekani nilioni 150 kwa mwaka, kitakapoanza uzalishaji.

Kiwanda kinachosubiri kujengwa ni cha nguo ambacho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mita milioni 240 kwa mwaka. Mhe. Waziri alieleza kuwa juhudi za kupata ekari 700 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho kwenye Wilaya ya Mkuranga zinaendelea na hivi karibibuni eneo hilo litakabidhiwa kwa wawekezaji hao.

Kwa upande wake, Dkt. Kian aliihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa China itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania ya kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Aidha, aliwakaribisha makampuni ya Tanzania kushiriki maonesho ya biashara yanayofanyika nchini China ili kuzitangaza bidhaa za Tanzania kwa madhumuni ya kupata soko nchini humo.

Mawaziri hao wawili waliweka saini Mkataba wa Makubaliano ya Kushirikiana katika masuala ya uchumi na teknolojia.



Wednesday, October 12, 2016

PRESS RELEASE


    
         
                           PRESS RELEASE 
SADC ORGAN TROIKA MINISTERIAL ASSESSMENT MISSION KINSHASA, DRC



The Southern African Development Community (SADC) Troika of the Organ on Politics, Defence and Security Cooperation undertook an assessment mission to the Democratic Republic of Congo (DRC) from 10th to 13th October 2016. The objective of the mission was to conduct an assessment of the political and security developments in the DRC aimed at assessing the on-going efforts related to peace and political stability of the DRC. H.E. John Pombe Joseph Magufuli, President of the United Republic of Tanzania in his capacity as the Chairperson of the Organ on Politics, Defence and Security cooperation mandated the Mission.

The assessment mission was led by Hon. Dr. Augustine P. Mahiga, Minister of Foreign Affairs and East African Cooperation of the United Republic of Tanzania and Chairperson of the Ministerial Committee of the Organ (MCO), who was accompanied by Hon. Georges Rebelo Chikoti, Minister of External Relations of the Republic of Angola and Deputy Chairperson of the MCO, Hon. Patricio Jose, Deputy Minister of National Defence of the Republic of Mozambique representing the outgoing chairperson of the MCO. The Mission was supported by the SADC Secretariat led by H.E. Dr. Stergomena Lawrence Tax, Executive Secretary of SADC. The mission also included SADC Ambassadors accredited in the DRC.

The Mission consulted with various stakeholders, including SADC Ambassadors accredited to the DRC, H.E. Edem Kodjo, African Union Facilitator of the National Dialogue, Hon. Raymond Tshibanda, Minister of Foreign Affairs and International Cooperation of DRC, Mr. Corneille Nangaa, and Mr. Nobert Katintima, Chairperson and Deputy of the Independent Electoral Commission (CENI) respectively, Senior Officials of the DRC Government, Representatives of Opposition Outside the  Dialogue (Rassemblement), Representatives of Opposition in the Dialogue, political parties in the Presidential majority led by Hon. Aubin Minaku, civil society and religious groups.

Following consultations and exchange of views with the various stakeholders, the Organ Troika Ministerial Mission:

1.   Noted the encouraging progress in the on-going AU-led National Dialogue and voters’ registration;

2.   Commended all stakeholders participating in the National Dialogue and noted progress made so far. Further urged all stakeholders who are not part of the National Dialogue to join the process;

3.   Encouraged all stakeholders to put the interest of the country and the people of the DRC first in the National Dialogue in order to ensure consensus on outstanding issues;

4.   Strongly condemned the violence that took place on 19th to 20th September 2016, which resulted in the loss of lives of innocent civilians and police officers as well as destruction of property. Further called on all stakeholders to act responsibly and avoid any actions that would result in any acts of violence;

5.   Strongly discouraged any attempts and threats that are aimed at undermining the process of Dialogue.

6.   Urged all stakeholders to create a conducive environment for free, fair democratic, peaceful, transparent and credible elections in the interest of peace, national unity, stability and socio-economic development of the country and to uphold the principles; ideals and aspirations of the Congolese people as enshrined in the Constitution and in accordance with SADC and AU principles and guidelines governing democratic elections;

7.   Urged all eligible Congolese voters to fully participate in the on-going voters registration process in order to exercise their democratic right as enshrined in the Constitution in the next elections;

8.   Called upon all stakeholders in the DRC, the international community and the Support Group to continue supporting the Africa Union-led National Dialogue and the electoral process, with a view to ensure sustainable peace, security and stability in the DRC; and

9.   Re-affirmed SADC’s support to the ongoing National Dialogue and pledged its full support to the final outcome.



Done in Kinshasa, Democratic Republic of Congo
12th October 2016