Friday, February 15, 2019
Thursday, February 14, 2019
Tanzania and Kazakhstan establish diplomatic relations
Ambassador Mero exchanges the signed communique with his counterpart, Ambassador Umarov. |
Ambassador Mero and Ambassador Umarov posing for a photo after signing a communique to establish diplomatic relations between the two countries. |
Wednesday, February 13, 2019
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Namibia nchini.
Mazungumzo yakiendelea. |
ZIARA YA PAMOJA YA NAIBU MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE NA FEDHA MPAKANI HOROHORO
Wadau walioshiriki ziara za Naibu mawaziri hao wakisikiliza wakati Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) akizungumza |
Sehemu nyingine ya wadau wakimsikiliza Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) |
Mkutano ukiendelea |
Wananchi wakipata huduma kwenye kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja |
Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Kijaji wakimsikiliza Bw. Bilali Juma, Afisa Mkemia wa kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Horohoro |
Dkt. Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na wadau mbalimbali |
Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja cha Horohoro kilihopo Mpakani mwa Tanzania na Kenya kama kinavyoonekana pichani |
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji wakiwa kwenye Nyumba iliyojengwa mpakani mwa Tanzania na Kenya. Horohoro. Mhe. Ndumbaro akiwa upande wa Kenya na Mhe. Kijaji akiwa upande wa Tanzania |
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji wakiendelea na ziara na kujionea alama za mipaka zilizopo mpakani hapo |
Mhe. Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Dkt. Kijaji wakiwa kwenye moja ya alama za mpaka |
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa ziara yao kwenye kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Horohoro |
Waandishi wa habari wakiwa kazini |
Waheshimiwa Naibu Mawaziri wakimsikiliza Mohamed Ibrahim anayesoma Darasa la nne Shule ya Vumba Kuu iliyopo Kenya. Mohamed alikuwa amerudi nyumbani kupata chakula wakati wa mapumziko mafupi kabla ya kurudi darasani. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
ZIARA YA PAMOJA YA NAIBU
MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE NA FEDHA MPAKANI HOROHORO
Watendaji wa Kituo Cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha
Horohoro kilichopo mkoani Tanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya wametakiwa
kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwa ya kukusanya mapato kwenye kituo hicho
yanafikiwa.
Kauli hiyo ilitolewa kwa pamoja na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb)
na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
walipotembelea kituo hicho tarehe 10 Februari 2019.
Dkt. Ndumbaro alishangazwa na mwenendo wa
ukusanyaji wa mapato wa kituo hicho ambapo takwimu zimekuwa zikipungua badala
ya kuongezeka kila mwaka. ‘Kwa miaka mitatu mfululizo takwimu za ukusanyaji wa
mapato ya kodi katika Kituo hiki zimekuwa zikishuka badala ya kupanda, jambo
ambalo si zuri kiuchumi na linakwenda kinyume kabisa na malengo ya Serikali ya
Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli’; Dkt. Ndumbaro
alimwambia Meneja wa TRA kituoni hapo.
Kwa mujibu wa takwimu hizo mwaka wa fedha
2017/2018, makusanyo ya kodi kwenye kituo hicho ni asilimia 81 ya malengo na
mwaka wa Fedha 2018/2019 inatarajiwa makusanyo yatafikia asilimia 76 ya malengo
yaliyowekwa.
Mhe. Naibu Waziri aliwataka watendaji hao kuwa
wabunifu kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali yanafikiwa bila kumuonea mtu
ikiwemo ubunifu wa kutatua changamoto zinazokikabili kituo hicho. Changamoto
hizo ni pamoja na ukosefu wa maji ambapo yananunuliwa kwa gharama ya Shilingi
milioni sita kwa mwezi. Naibu Waziri alishangazwa na uamuzi huo wa kutumia
fedha nyingi kwa ajili ya maji wakati kuchimba kisima hakiwezi kugharimu zaidi
ya milioni 10.
Dkt. Ndumbaro pia hakuridhishwa na ubora wa jengo
la kituo hicho na kubainisha kuwa ndio sababu zinazofanya kituo hicho
kutozinduliwa rasmi hadi leo.
Kwa upande wake, Dkt. Kijaji alisikitishwa na
utendaji usiokuwa na kiwango wa mamlaka zote zilizopo kwenye kituo hicho na
kusisitiza kuwa, kwa kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ipo chini ya himaya
yake atachukua hatua zinazostahili. Moja ya maeneo yenye udhaifu katika kituo
hicho ni uchukuaji wa takwimu zikiwemo za magari yanayoingia na kutoka ambapo
kila mamlaka iliyopo hapo ina takwimu tofauti.
Aidha, Mhe. Kijaji alipiga marufuku kwa
wafanyabiashara wa Wilaya ya Mkinga kwenda Wilaya ya Muheza kufuata huduma za
kodi zikiwemo za kulipia kodi mbalimbali. Mhe. Naibu Waziri alimuagiza Mkuu wa
Wilaya ya Mkinga kuwatangazia wafanyabiashara wa Mkinga marufuku hiyo na
kuagiza watumishi wa TRA wa Mkoa kwenda Mkinga kutoa huduma za kikodi angalau
mara tatu kwa wiki.
Kuhusu ubora wa jengo hilo, Dkt. Kijaji aliagiza
apatiwe nyaraka za jengo hilo ifikapo tarehe 15 Februari 2019 ili aone majukumu
ya kila mmoja katika ujenzi wa jengo hilo kwa madhumuni ya kuchukua hatua
stahiki.
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji walifanya
ziara ya pamoja kwenye kituo hicho cha Horohoro kwa lengo la kujionea
changamoto ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.
13 Februari
2019
|
Tuesday, February 12, 2019
Job Announcement at the Commonwealth Secretariat
PRESS RELEASE
Job Announcement at the Commonwealth Secretariat
The Ministry
of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy
notification from the Commonwealth Secretariat inviting qualified Tanzanians to
apply for the post of Legal Adviser (Natural Resources) available
at the Commonwealth Secretariat.
In line with the Commonwealth’s commitment to gender equality, the Commonwealth Secretariat encourages applications from appropriately qualified women for this post.
Application
details can be found on the Secretariat’s website, http://thecommonwealth.org/jobs. Closing date for application is Wednesday
20th February, 2019 at 17:00 GMT.
Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
12th February 2019.
|
Saturday, February 9, 2019
Tanzania na Azerbaijan kuanzisha Ushrikiano wa Kidiplomasia
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Modest J. Mero (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi wa Kudumu wa Azerbaijan katika Umoja wa Mataifa, Balozi Yashar Aliyev jijini New York Marekani. Viingozi hao walikutana kwa ajili ya kusaini Makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Mataifa yao. |
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Modest J. Mero (kulia) na Mwakilishi wa Kudumu wa Azerbaijan katika Umoja wa Mataifa, Balozi Yashar Aliyev wakiweka saini Makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Azerbaijan jijini New York, Marekani. Wengine katika picha ni maafisa wa ofisi za Balozi, Bi, Lilian A. Mukasa na Bw. Tofig F. Musayev. |
Balozi Mero na Balozi Aliyev wakiagana baada ya kusaini makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya mataifa yao. |
Friday, February 8, 2019
Naibu Mawaziri watembelea Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Mtukula.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Julius Wandera Maganda katika Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja mpakani cha Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda Tarehe 7 Februari 2019. Mara baada ya kukutana walipata fursa ya kutembelea na kujionea namna kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani cha Mtukula (OSBP) kinavyofanya kazi na kufanya Mkutano wa pamoja uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka Tanzania na Uganda. Mkutano huo umefanyia Mpakani mwa Tanzania na Uganda eneo la Mtukula. |
Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Waganda kabla ya kufanya mkutano wa pamoja na wadau mbalimbali. Wengine katika picha ni wajumbe walioongozana na Naibu Mawaziri hao. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.Ndumbaro (Mb.) akizungumza kwenye Mkutano na wadau mbalimbali pamoja na jumuiya ya wafanya biashara walio hudhuria mkutano huo. |
Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Maganda naye akizungumza na wadau pamoja na jumuiya ya wafanya biashara walio hudhuria mkutano huo |
Wadau kutoka upande wa Tanzania wakisikiliza kwa makini wakati Naibu Mawaziri, Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Maganda walipokuwa wakizungumza kwenye mkutano uliyofanyika mpakani wa Tanzania na Uganda-Mtukula |
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwa na Mhe. Maganda wakisikiliza kwa makini michango mbalimbali ya wadau iliyokuwa ikiwasilishwa kwenye mkutano. |
Mwakilishi wa jumuiya ya wafanya biashara akichangia mada kwenye mkutano Mmbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Uganda naye akichangia mada wakati wa mkutano huo ukiendelea. |
Ujumbe wa Uganda nao wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini. |
Viongozi wa pande zote mbili walipata fursa ya kuzungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo na kuwaelezea yaliyojiri kwenye mkutano. |
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano. |
Viongozi hao wakifanya ziara kwenye maeneo mbalimbali ya kituo hicho cha pamoja na kujione namana watendaji wanavyo fanya kazi kwa umakini kwa kutumia vifaa vya kisasa katika kupambana na mambo mbalimbali ikiwemo namna ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko. |
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakimsikiliza Afisa wa ukusanyaji mapato kutoka Tanzania Bw. Mohamed Shamte alipokuwa akielezea namna kituo hicho cha pamoja kinavyo fanya kazi. Naibu Mawaziri hao walijione namna watendaji wanavyofanya kazi kwa umakini kwa kutumia vifaa vya kisasa katika kupambana na mambo mbalimbali, ikiwemo udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola.. |
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Julius wakiendelea na kukagua Kituo ili kujionea namna watendaji wake wanavyotoa huduma kwa wananchi wa pande zote mbili. |
Katika picha ni jengo la Kituo cha kutolea hudmua kwa pamoja Mtukula mpakani mwa Tanzania na Uganda. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Akiainisha mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kituo hicho , Dkt. Ndumbaro alieleza namna mizigo mbalimbali ikipita kwa wakati kwa kuzingatia taratibu zote zilizopo pamoja na wafanyabiashara kati ya nchi hizi mbili wakifanya biashara zao bila vikwazo vyovyote vile.
Pamoja na mambo mengine Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kuwajulisha wadau mbalimali waliohudhuria mkutano huo, kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeanzisha safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kutoka Dar es Salaam, Arusha mpaka Enttebe, Uganda. Mafanikio hayo yametokana na mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyopo baina ya Tanzania na Uganda na pia kupitia Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Mhe Maganda, alifurahishwa na hali ya kituo hicho namna huduma zinavyotolewa. Aidha, aliahidi kuwa Serikali ya Uganda itaongeza watendaji kazi kwenye kituo hicho ili kuwezesha upande wa Uganda kufanya kazi masaa 24 kama ilivyo kwa upande Tanzania. Pia alisisitiza nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya Ushirikiano.
Pia katika Mkutano huo wadau walitoa pongezi kwa viongozi wa Serikali za pande zote mbili kwa kuanzisha kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Mtukula, ambapo walisema kuanzishwa kituo hicho kumeongeza chachu ya maendeleo kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili ambapo wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao kwa wingi bila kupata changamoto kulinganisha na hapo awali kabla ya kuanzishwa kwa kituo hicho.
Kadhalika wadau walitoa pongezi kwa watendeji waliopo kituoni hapo kwa upande wa Tanzania, kwa kutoa huduma nzuri kwa masaa 24 kwenye kituo hicho ambapo, imepelekea wafanyabiashara kutokupoteza muda mwingi wafikapo mpakani hapo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
9 Februari 2019
|
Subscribe to:
Posts (Atom)