Monday, September 23, 2019

PROF. KABUDI ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI UNAOENDELEA NEW YORK - MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu mabadiliko ya tabianchi unaofanyika wakati wa kikao cha 74 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa New York, Marekani. Mbali kulia kwa Waziri Kabudi ni Rais wa Marekani Mhe. Donald Trump akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mhe. Mike Pompeo. Wengine ni Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) Mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu ulinzi na usalama na Balozi na mwakilishi  wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Modest Mero.

NAIBU KATIBU MKUU AMUAGA BALOZI WA QATAR

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani M. Mwinyi akimkaribisha Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi ambaye amemaliza muda wake wa utumishi wakati alipowasilis katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam. Aidhaa, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, uwekezaji baina ya Tanzania na Qatar. 

Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Mhe. Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani M. Mwinyi wakati walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani M. Mwinyi akimsititizia jambo Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi ambaye amemaliza muda wake wa utumishi wakati walipokuwa na mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo Jijini Dar es Salaam.


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akutana, kumuaga Balozi wa Qatar nchini Tanzania 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani M. Mwinyi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi.

Akiongea wakati wa hafla ya kumuaga Balozi huyo wa Qatar iliyofanyika Dar es Salaam Balozi Mwinyi amemshukuru Balozi Al-Madadadi kwa kumaliza muda wake wa uwakilishi na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha mahusiano kati ya Tanzania na Qatar katika kipindi chake cha uwakilishi. 

Aidha, Katibu Mkuu ameelezea kwamba yapo maeneo ambayo nchi za Tanzania na Qatar zitaendelea kushirikiana kwa ukaribu pamoja na maeneo mengine ikiwemo biashara na uwekezaji. 

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Al-Madadadi ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano wa kutosha wakati wa kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.

Mhe. Balozi ameeleza kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Qatar na amepongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha mahusiano hayo.  

Pia amepongeza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza uchumi wa nchi,kuongeza uwajibikaji katika serikali za umma na mapambano dcidi ya rushwa.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar Es Salaam,Tanzania
23 Septemba 2019
  



PROF. KABUDI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU MSAIDIZI WA RAIS WA MAREKANI NA MKURUGENZI MWANDAMIZI WA MASUALA YA AFRIKA BI ERIN WALSH.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin  Walsh. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York,Marekani. Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia,kiuchumi na kisiasa baina ya Tanzania na Marekani. Viongozi hao wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha mahusiano yaliyopo katika nyanja mbalimbali kwa faida ya Nchi hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin  Walsh. Pamoja nao ni Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Wilson Masilingi akifuatilia mazungumzo hayo.
Balozi na Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Modest Mero (katikati) akifuatilia mazungumza ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin  Walsh.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiagana na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin  Walsh baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York,Marekani.






Sunday, September 22, 2019

MHE. MAKAMU WA RAIS AFUNGUA RASMI TAMASHA LA NNE LA SANAA NA UTAMADUNI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Septemba 2019 kwa ajili ya kufungua rasmi Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama JAMFEST 2019. Wengine katika picha ni pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza. Tamasha la mwaka huu limebeba kaulimbiu isemayo "Uanuai wa Kitamaduni: Msingi wa Utangamano wa Kikanda, Maendeleo ya Kiuchumi na Kukuza Utalii".

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Makamu wa Rais ametoa rai kwa wananchi wa Afrika Mashariki kuuenzi utamaduni wao ambao ni tunu kubwa kwa kuurithisha kwa vizazi vyao. Pia alitumia fursa hiyo kueleza kuwa, utamaduni ni nyenzo muhimu ya kuleta umoja, amani, ushirikiano na upendo miongoni mwa wana Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pia sanaa na ubunifu ni sekta inayokua haraka na imetengeneza ajira kwa wingi kwa vijana na kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi za Jumuiya ya Mashariki  ikiwemo Tanzania. Mhe. Makamu wa Rais aliongeza kuwa, Tamasha la JAMAFEST tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013 limekuwa ni chachu ya kuimarisha mtangamano. Zaidi ya washiriki 3000 kutoka Nchi Wnachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanashiriki Tamasha hilo.
Mhe. Makamu wa Rais akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga ngoma kuashiria ufunguzi rasmi wa Tamasha hilo ambalo alitangaza kuwa linakwenda sambamba na Tamasha la Urithi la Tanzania. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mhe. Mwakyembe (kulia), Waziri wa Michezo wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed (kushoto) na  Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Stephen Mlote (mwenye tai nyekundu kushoto)
Wananchi wa Dar es Salaam wakifuatilia matukio wakati wa ufunguzi rasmi wa Tamasha la Nne la JAMAFEST
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akizungumza wakati wa Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki huku wanachi wakimsikiliza
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Tanzania, Bw. Peter Msechu akiwaobgoza wasanii wenzake kuimba wimbo maalum kuhusu JAMAFEST 2019
Mhe. Makamu wa Rais na Viongozi waliokuwa meza kuu wakiwa wamesimama kwa heshima wakati wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiimbwa wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST 2019
Kikundi cha ngoma kutoka Tanzania kikitumbuiza
Kikundi cha ngoma kutoka Rwanda kikitumbuiza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kikundi cha ngoma kutoka Burundi kikitumbuiza
Kikundi cha ngoma kutoka Kenya kikitumbuiza kwenye JAMAFEST 2019
Kikundi cha ngoma kutoka Uganda kikitumbuiza kwenye JAMAFEST 2019
Mhe. Makamu wa Rais akiagana na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Bw. Nasib Abdul maarufu kama Diamond ambaye alitumbuiza kwenye Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Afrika Mashariki

PROF.KABUDI AWASILI NEW YORK MAREKANI KUSHIRIKI MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA

Balozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa,Balozi Modest Mero (Kulia) akitoa maelezo kuhusu Mkutano wa 74 wa Baraza la kudumu la Umoja wa Mataifa kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (hayupo pichani) utakaofanyika New York Marekani kuanzia September 21,2019 hadi September 30,2019.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (kushoto) na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Wilson Masilingi wakifuatilia maelezo ya Balozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa,Balozi Modest Mero mara baada ya kuwasili New York,Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiandika jambo wakati akipatiwa maelezo na Balozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa,Balozi Modest Mero (hayupo picha)kuhusu Mkutano wa 74 wa Baraza la kudumu la Umoja wa Mataifa unaofanyika New York Marekani kuanzia September 21,2019 hadi September 30,2019. Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Wilson Masilingi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipitia moja ya nyaraka kuhusu Mkutano wa 74 wa Baraza la kudumu la Umoja wa Mataifa unaofanyika New York Marekani kuanzia September 21,2019 hadi September 30,2019.
Baadhi ya wajumbe na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (hayupo pichani) wakati akipewa maelezo mbalimbali kuhusu Mkutano wa 74 wa Baraza la kudumu la Umoja wa Mataifa unaofanyika New York Marekani kuanzia September 21,2019 hadi September 30,2019. Wakwanza kulia ni Balozi Mteule Bujiku Sakila,mshauri wa Rais kuhusu masuala ya diplomasia.
Baadhi ya wajumbe na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (hayupo pichani) wakati akipewa maelezo mbalimbali kuhusu Mkutano wa 74 wa Baraza la kudumu la Umoja wa Mataifa unaofanyika New York Marekani kuanzia September 21,2019 hadi September 30,2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika kikao kazi na baadhi ya Mabalozi pamoja na Ujumbe aliombatana nao kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 74 wa Baraza la kudumu la Umoja wa Mataifa unaofanyika New York Marekani kuanzia September 21,2019 hadi September 30,2019. 



Saturday, September 21, 2019

MAKAMU WA RAIS KUFUNGUA RASMI TAMASHA LA UTAMADUNI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI




Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa pamoja na viongozi wengine kutoka Tanzania na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuyapokea maandamano ya vikundi mbalimbali vya sanaa na utamaduni vitakavyoshiriki Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama JAMAFEST litakalofunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam tarehe 22 Septemba 2019.
Maandamano ya vikundi vya utamaduni kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yakipita mbele ya mgeni rasmi 
Umati wa wananchi uliojitokeza kujionea vikundi mbalimbali vya utamaduni kuelekea ufunguzi rasmi wa Tamasha la Nne la JAMAFEST hapo tarehe 22 Septemba 2019

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota (mwenye suti) akiwa na Maafisa kutoka Wizara na wadau wengine wakati wa maandalizi ya ufunguzi rasmi wa Tamasha la Nne la JAMAFEST utakaofanyika tarehe 22 Septemba 2019

Wadau mbalimbali
Kikundi kutoka Burundi

 

Kikundi kutoka Kenya
Kikundi kutoka Rwanda
Kikundi kutoka Tanzania
Kikundi kutoka Uganda
Wadau kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifurahia kukamilika kwa maandalizi kabla ya ufunguzi rasmi wa JAMAFEST tarehe 22 Septemba 2019
==============================================================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makamu wa Rais kufungua Tamasha la Nne la Utamaduni la Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua rasmi Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival (JAMAFEST) litakalofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 hadi 28 Septemba 2019.

Tamasha hilo ambalo limebeba kauli mbiu isemayo “Cultural diversity: A key Driver to Regional Intergration, Economic Growth and Promotion of Tourism” linalenga kuwa jukwaa la kuonesha utamaduni wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi hizo kutumia fursa hii kama njia mojawapo  ya kuwaleta pamoja viongozi na wananchi wa Afrika Mashariki pamoja ili kusherehekea utajiri wa utamaduni uliopo.

Aidha, kufanyika kwa JAMAFEST hapa Tananzania kutawezesha ushiriki mkubwa wa wananchi na hii ni fursa adhimu ya kutangaza mila, utamaduni na Sanaa za Tanzania kwa Wana Afrika Mashariki. Pia Tanzania itatumia nafasi hiyo kutangaza utalii wa kitamaduni uliopo pamoja na wananchi kunufaika kiuchumi kupitia biashara mbalimbali zitakazofanyika wakati wa Tamasha hilo.

Akizungumza wakati wa kutangaza kukamilika kwa maandalizi ya Tamasha hilo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alitoa wito kwa wananchi wa Tanzania hususan wakazi wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya uwepo wa Tamasha hili ili kunufaika nalo. 

Alisema kuwa, nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimetuma vikundi mbalimbali vya Sanaa na utamaduni kwa ajili ya kushiriki tamasha hilo la aina yake. Aidha, alisema kuwa fursa hii ni muhimu kwa Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuuonesha ulimwengu urithi mkubwa wa utamaduni uliopo miongoni mwao.

Vilevile, alitoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaa kujitokeza kwa wingi, bila kukosa kwenye sherehe za ufunguzi wa Tamasha hilo zitakazofanyika kwenye Uwanja wa Taifa tarehe 22 Septemba 2019.

Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na mambo mengine litaangazia shughuli mbalimbali za kitamaduni na sanaa zitakazofanyika Uwanjani hapo ikiwa ni pamoja na: Midahalo na Warsha; Maonesho ya Sanaa za uoni, Uoneshaji na Ushindanishaji wa Filamu, Masoko ya Sanaa na Ubunifu, Michezo ya Watoto, Michezo ya Jadi, Soko na Maonesho ya Vyakula vya asili, Maonesho ya Mavazi na Ulimbwende na Ziara, Tuzo na Utalii kwa washiriki.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa waratibu wa Tamasha hilo ambalo linashirikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda na Sudan Kusini.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
21 Septemba 2019

Thursday, September 19, 2019

Tanzania, Poland zakubaliana kuongeza ushirikiano katika biashara
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zimekubaliana kuongeza ushirikiano katika biashara, na kuwataka wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara.
Makubaliano hayo yalifanyika Jijini Dar es Salaam jana (Septemba 20, 2019) ambapo serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi ili hali Poland iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Marcin Przydacz.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya makubaliano hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa lengo la makubaliano hayo ni kukuza ushirikiano uliopo kati ya nchi hizi.
"Kwa sasa, tunashirikiana na Poland katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na biashara ambayo takwimu zinaonesha kwamba biashara kati ya Tanzania na Poland zimepanda kutoka milioni 77.7 mwaka 2016 mpaka milioni 124.5 mwaka 2017. Bidhaa za Tanzania zinazouzwa Poland ni pamoja na chai, kahawa na tumbaku. Tanzania inanunua Poland bidhaa mbalimbali kama tairi za magari, vifaa vya maabara na vifaa vya umeme," alisema Prof. Kabudi  
Prof. Kabudi aliongeza kuwa, fursa za biashara baina ya nchi hizi mbili bado ni nyingi na imekubaliwa kuwa balozi zetu na taasisi zingine za Serikali zetu zitumike kuongeza ushirikiano katika biashara. "Kwa hili, tunawaomba wafanyabishara wetu kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara," Aliongeza Prof. Kabudi

Kwa mujibu wa Waziri Kabudi, Tanzania na Poland zinashirikiana kwenye miradi mikubwa miwili. Mradi wa kwanza ni wa kiwanda cha kuunganisha trekta, kilichopo Kibaha ambao unatekelezwa kwa mkopo wa riba nafuu kutoka Serikali ya Poland. Kupitia mradi huu, jumla ya trekta 2400 zinaunganishwa nchini kupitia kampuni ya URSUS ya Poland. Tayari trekta 875 zimeshaunganishwa. Mradi huu utaongeza uzalishaji kwenye sekta ya kilimo na kuleta mapinduzi ya kilimo kutoka kutumia jembe la mkono kwenda kutumia trekta.

Mradi mwingine ni ule wa kujenga maghala ya kuhifadhia nafaka ambapo jumla ya maghala 8 yanajengwa katika kanda zote zinazohifadhi chakula nchini. Mradi huu utaongeza uwezo wa Serikali wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 250,000 kwa sasa hadi tani 500,000. 

Katika hatua nyingine, tumekubaliana pia kutoa fursa ya elimu ambapo watanzania sasa watapata fursa ya kwenda kusomaPoland ambapo fursa nyingi zitatolewa katika fani ya udaktari wa aina mbalimbali, uhandisi, sayansi, Tehama, kilimo na maeneo mengine. 


Prof. Kabudi aliongeza kuwa, Tanzania imeendelea kuvutia watalii kutoka nchi ya Poland. Kila mwaka, watalii wapatao 12,000 wamekuwa wakitembelea visiwa vya Zanzibar kwa ndege zinazotoka miji mbalimbali ya Poland moja kwa moja mpaka Zanzibar. Idadi ya watalii inaendelea kuongezeka kutoka watalii 12,241 mwaka 2017 hadi watalii 18, 853 mwaka 2018.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Marcin Przydacz amesema kuwa Serikali yake itaendelea kuwahimiza Wapoland kuja kuwekeza nchini kwa wingi na hasa kwenye maeneo ya uzalishaji wa dawa, kilimo hususan katika uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo, uzalishaji wa mashine za viwandani na uzalishaji wa bidhaa za viwandani.

Pia, Waziri Przydacz ameahidi kuwa Serikali yake itaendeleea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayooongozwa na Mhe. Rais Magufuli ya kutafuta suluhisho la changamoto ya uhaba wa maji inayokabili wananchi sehemu mbalimbali nchini. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Yokohama, Japan
19 Septemba, 2019

PROF. KABUDI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe. Marcin Przydacz. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na

Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) pamoja na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe. Marcin Przydacz (hayupo pichani)

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe. Marcin Przydacz pamoja na ujumbe alioambatana nao wakimsikiliza Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)(hayupo pichani)
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe. Marcin Przydacz wakiwa katika mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara
 ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya picha ya kuchora ya Mlima Kilimanjaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe. Marcin Przydacz mara baada ya mazungumzo rasmi waliyoyafanya kaaika ofisi neogo za Wizara ya Mambo ya 

Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.