Na. OWM, ZANZIBAR
“Tatizo la athari za maafa
yanayotokana na majanga ya asili linahitaji ushiriki wa sekta zote ili kukabiliana
nalo ipasavyo, katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”
Mwaluko.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Zanzibar na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy
Mwaluko wakati alipokuwa anafungua kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye
dhamana ya maafa katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambaye
yeye ni mwenyekiti.
Mwaluko amesema nchi zote za SADC zina uzoefu
wa masuala ya maafa, hivyo ni matarajio yake kuwa kazi waliyopewa ya kuandaa
nyaraka kwa ajili ya mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya maafa utakaofanyika
siku ya Ijumaa tarehe 21 Februari 2020, uweze
kufikia malengo yake.
Katika kikao hicho, Makatibu Wakuu
wataandaa nyaraka itakayo ainisha mikakati na programu za kukabiliana na maafa
na mpango unaobainisha namna nchi za SADC zilivyojipanga kukabiliana na maafa
yanapotokea katika ukanda huo.
Kwa upande wake, Naibu Katibu
Mtendaji wa SADC wa Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda, Dkt. Thembinkosi
Mhlongo alieleza kuwa athari za maafa
zikiwemo vifo, uharibifu wa mali na miundombinu zimezikumba takribani nchi zote
za SADC. Hivyo amesisitiza umuhimu wa nchi hizo kushirikiana kwa pamoja kuandaa
mikakati ya menejimenti ya maafa.
Naye, Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Bw. Abdallah Hassan Mitawi amewaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa nchi za SADC zimelipa
umuhimu mkubwa suala la kukabiliana na athari za maafa na hilo linadhihirishwa
na ushiriki wa nchi 15 kati ya 16 wanachama wa SADC katika mkutano huo.
Mkutano huo unaofanyika kwenye Hoteli
ya Madinat AL Bahir iliyopo Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar unatarajiwa
kuhitimishwa kwa kikao cha ngazi ya Mawaziri tarehe 21 Februari 2020 ambapo
Mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.
Dkt. Ali Mohamed Shein.
“Ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza
madhara ya maafa ni njia bora ya kujenga Uhimili katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”
MWISHO.
|
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akifafanua umuhimu wa ushiriki wa
kisekta kwenye Kupunguza madhara ya maafa, wakati akifungua kikao cha SADC cha
Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo yeye ni mwenyekiti wa
kikao hicho, leo tarehe 18 Februari 2020, Zanzibar.
|
|
Naibu Katibu Mtendaji wa SADC wa Masuala ya
Ushirikiano wa Kikanda, Dkt. Thembinkosi Mhlongo akifafanua umuhimu wa
Nchi za SADC kuwa na mikakati ya
kukabili maafa yanayo zikabili, wakati wa kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu
wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC, leo tarehe 18 Februari, 2020, Zanzibar |
|
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais, Zanzibar, Bw. Abdallah Hassan Mitawi akifafanua namna ya nchi za SADC zinavyoathirika
na maafa ya asili, wakati wa kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya
maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC, leo tarehe 18 Februari, Zanzibar |
|
Baadhi ya makatibu wakuu kutoka Tanzania,
wakifuatilia kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika
ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC, leo tarehe
18, Februari, 2020, Zanzibar, (katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi,anayeshughulikia Mifugo, Profesa
Olesante Ole Gabriel (kulia kwake), Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
kujenga Taifa, Dkt. Faraij Mnyepe, na
Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.
|
|
Baadhi ya maafisa waandamizi kutoka
ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC),
wakifuatilia kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa, leo
tarehe 18 Februari, 2020, Zanzibar.
|
|
Baadhi ya maafisa waandamizi kutoka ukanda wa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia
kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa, leo tarehe 18
Februari, Zanzibar, Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe,(kulia), Mkurugenzi wa Kamisheni ya Kukabiliana na
Maafa, Zanzibar , Makame Khatibu Makame na Naibu Mkurugenzi wa Kamisheni hiyo,
Muhidin Ali Muhidin |
|
Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa
katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, leo
tarehe 18, 2020, ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ushiriki wa kisekta
kwenye Kupunguza madhara ya maafa ni
njia bora ya kujenga Uhimili katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC)”
|
|
Makatibu Wakuu na maafisa waandamizi wenye
dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika (SADC,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa
mkutano huo, leo tarehe 18, Februari, 2020, ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni
“Ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara
ya maafa ni njia bora ya kujenga
Uhimili katika ukanda wa nchi wanachama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC)”
|