Na Mwandishi Wetu
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaongoza viongozi
waandamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwemo Rais Dkt Hussein Ali
Mwinyi kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli huku baadhi ya mabalozi
wakibubujikwa na machozi.
Rais Samia
Suluhu Hassan amesaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Kamrijee Dar es
Salaam mchana wa leo na kufuatiiwa na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi
zao hapa Tanzania kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 katika
hospitali ya Mzena kwa maradhi ya moyo.
Pia Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Hussein Ally Mwinyi nae pia
amesaini kitabu cha maombolezo akifuatiwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe Othaman Masoud
Baadhi ya
Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Nchini walishindwa kujizuia na kutokwa
na machozi kumlilia Hayati Dkt. Magufuli na kumuelezea kuwa alikuwa kiongozi
jasiri na mzalendo si kwa manufaa ya Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla ambapo
Balozi wa Jamaica hapa nchini Mhe. Velisa Delfosse amemuelezea Hayati Dkt
Magufuli kama mwanampinduzi na mzalendo halisi wa Afrika wa wakati huu
“Rais Magufuli
alikuwa mwanampinduzi na mzalendo halisi wa Afrika wa wakati huu, kwa kweli
tumeguswa sana na msiba wake hakika pengo lake halitazibika, tunamuombea kwa
Mungu apumzike salama,” Amesema Balozi Delfosse
Nae Balozi wa
China hapa Nchini Mhe. Wang Ke mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo
amemuelezea Hayati Magufuli kama kiongozi mwenye maono na mzalendo mwaminifu
kwa Afrika,na kwamba atakumbukwa na Watanzania kwa jitihada zake kubwa za
kuleta mabadiliko chanya ili kuinua hali
ya maisha hususani wale wa kipato cha chini.
Kwa upande
wake Balozi wa Sudani ya Kusini Mhe. William Ruben amewasihi viongozi wa Afrika
na Watanzania kwa ujumla kufuata nyayo za Hayati Dkt Magufuli kwa kuwa alikuwa
alama halisi ya Afrika na alitufundisha wengi wetu kuamini kuwa Afrika
imebarikiwa na ni tajiri kinyume na tulivyoamini kuwa tunahitaji msaada kutoka kwa
mataifa ya nje ya bara la Afrika
“Naomba
kuwasihi viongozi wa Afrika na Watanzania kwa ujumla kufuata nyayo za Hayati
Dkt Magufuli kwa kuwa alikuwa alama halisi ya Afrika na alitufundisha wengi
wetu kuamini kuwa Afrika imebarikiwa na ni tajiri kinyume na tulivyoamini kuwa
tunahitaji msaada kutoka kwa mataifa ya nje ya bara la Afrika,” Amesema Balozi
Ruben
Mabalozi
wengine waliofika katika viwanja vya Karimjee na kusaini kitabu cha maombolezo
ni pamoja na Balozi wa Morocco Mhe. Abdililah Benryane, Balozi wa Ethiopia Mhe
Yonas Sanbe, Balozi wa Qatar Mhe Abdulla Jassim Al Madadadi, Balozi wa Japan
Mhe Shinichi Goto Balozi wa Palestina Mhe Derar Ghannan, Balozi wa Cuba Mhe
Lucas Damingo, Balozi wa Pakistan Mhe Mohammed Salem, Balozi wa Uswis Mhe Didier
Chassot, Balozi wa Ireland Mhe Mary Oneill.
Wengine ni
Balozi wa Rwanda Meja Jeneral Charles Karamba, Balozi wa Syria Dr Sawsan Alani,
Balozi wa Korea Mhe Kim Yong Su, Balozi wa Iran Mhe Hussein Alvandi Behined, Balozi
Hispania Mhe Fransisca Pedros, Balozi
wa Zambia nchini Mhe. Benson Chali na Balozi
Vietnam Mhe Nguyen Namtien.
Baadhi ya
Wakuu wa mashirika na Taasisi za Kimataifa waliofika kusaini kitabu cha
maombolezo ni pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Mhe. Zlatan Milisic,
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF,
Mhe. Shahini Bahuguna,Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu,sayansi na utamaduni
Mhe Tirso Do Santos,Shirika la Kazi duniani Wellingtone Chibebe,Shirika la
Maendeleo la Umoja wa mataifa Mhe Christine Musisi na Shirika la kuhudumia
wakimbizi la Umoja wa Mataifa Mhe Antonio Jose Canandula.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu
cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee
kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021 jijini
Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima
mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee
kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021 jijini Dar es
Salaam
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisaini
kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea
tarehe 17 Machi 2021 jijini Dar es Salaam
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Othman Masoud akisaini
kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Balozi
wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto akisaini kitabu cha maombolezo
katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Balozi
wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Benson Chali akisaini kitabu cha maombolezo
katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Balozi
wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Mary O’neill kisaini kitabu cha maombolezo
katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Mratibu
Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN) Zlatan Milisic akisaini kitabu cha
maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Christine Musisi akisaini
kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Balozi
Hispania Mhe Fransisca Pedros akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya
Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Balozi
wa Rwanda Meja Jeneral Charles Karamba akisaini
kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Karimjee kufuatia kifo cha aliyekuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli