Thursday, June 15, 2023

MAHAKAMA YA AFRIKA YAISHUKURU SERIKALI YA TANZANIA

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud kutoka Tanzania ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa misaada inayoipatia mahakama hiyo ikiwemo ujenzi wa jengo la ofisi ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilikabidhi eneo la ujenzi kwa Mkandarasi CRJE jijini Arusha tarehe 02 Juni 2023.

 

Jaji Aboud ametoa shukrani hizo wakati wa kikao na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb) kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 15 Juni 2023.

 

Rais wa Mahakama ya Afrika na watumishi wengine, wakiwemo Makamu wa Rais; Majaji na Msajili wapo jijini Dodoma kwa ajili ya kikao (retreat) cha kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Mahakama hiyo ili kubaini mafanikio na changamoto kwa ajili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

 

Kwa kutumia fursa ya kikao kufanyika Dodoma, Rais na ujumbe wake wametumia nafasi hiyo kukutana na wadau mbalimbali ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ili kajadili utekelezaji wa majukumu ya chombo hicho muhimu barani Afrika.

 

Kwa upande wake, Mhe. Waziri Dkt. Tax alieleza kufurahishwa na uamuzi wa Mahakama hiyo wa kufanya kikao chao jijini Dodoma ambapo ni makao makuu ya nchi. Aidha, aliwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano unaohitajika ili mahakama hiyo iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa jengo la Ofisi.

 

Mhe. Waziri Dkt. Tax alihitimisha mazungumzo yake kwa kumpongeza Jaji Aboud kwa kuchaguliwa tena kwa kipindi cha awamu ya pili na cha mwisho cha miaka miwili kuwa Rais wa Mahakama hiyo. Jaji Aboud alichaguliwa wakati wa ufunguzi wa Baraza la 69 la Pan-Afrika lililofanyika Arusha tarehe 12 Juni 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa Mkutano kati yake na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud (hayupo pichani) alipomtembelea Ofisi kwake jijini Dodoma tarehe 15 Juni 2023. Mhe. Jaji Imani na ujumbe wake, wakiwemo Makamu wa Rais; Majaji na Msajili wapo jijini Dodoma kwa ajili ya kikao cha kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Mahakama hiyo ili kubaini mafanikio na changamoto kwa ajili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa Mkutano kati yake na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud (kshoto) alipomtembelea Ofisi kwake jijini Dodoma tarehe 15 Juni 2023. Kulia ni Makamu Rais wa Mahakama hiyo, Mhe. Jaji Sacko Madibo
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud akizungumza wakati wa Mkutano kati yake na Mhe. Dkt. Tax (hayupo pichani)
Mkutano ukiendelea
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Levina Maleo akizungumza wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Waziri Dkt. Tax na Mhe. Jaji Aboud hawapo pichani
Afisa kutoka Kitengo cha Sheria, Bi. Elizabeth Bukwimba akichangia jambo wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Jaji Aboud hawapo pichani
Mhe. Jaji Aboud akimpatia Mhe, Dkt. Tax zawadi ya nembo ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao
Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Jaji Aboud wakijadili jambo baada ya mazungumzo yao
Picha ya pamoja 
Picha ya pamoja

TANZANIA YAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA URUSI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Serikali ya Urusi kuwekeza nchini kwa maslahi ya pande zote mbili na ustawi wa dunia kwa ujumla.

Mwaliko huo umetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) wakati aliposhiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi jana jioni Jijini Dar es Salaam. 

“Tanzania ina mazingira tulivu ya biashara na uwekezaji yanayotoa fursa za uwekezaji, hivyo natoa rai wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Urusi kuja kuwekeza Tanzania ili kuimarisha zaidi biashara baina ya nchi zetu mbili,” alisema Balozi Mbarouk

 Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Tanzania kwa kushirikiana na sekta binafsi zimeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuhakikisha kuwa uwekezaji unafanyika katika mazingira rafiki na salama na kuwafanya wafanyabiashara kutoka nje kufanya biashara zao katika mazingira salama na rafiki. 

Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Urusi imekuwa mshirika wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kiteknolojia na kisiasa nchini Tanzania. Kwa kusainiwa kwa mkataba wa kuanzisha Tume ya Pamoja ya Kiserikali ya Biashara na Ushirikiano wa Kiuchumi, nchi hizo mbili zipo katika nafasi nzuri zaidi ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande zote mbili.

Kwa upande wake Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan alisema kuwa ushirikiano wa Urusi na Tanzania ni wa kihistoria na umekuwa imara wakati wote. Urusi itaeendelea kushirikiana na Tanzania kijamii, kisiasa na kiuchumi wakati wote.

“Tunapoadhimisha siku hii muhimu tunakumbuka pia miaka 62 ya uhusiano kati ya Urusi na Tanzania. Aidha, Balozi Avetisyan aliongeza kuwa Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuendeleza ushirikiano wa kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya pande zote mbili,” alisema Balozi Avetisyan.

“Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania kuboresha biashara na uwekezaji ambapo kwa sasa ukuaji wa biashara baina ya mataifa yetu umeongezeka. Tunaendelea kuboresha biashara licha ya changamoto zinazojitokeza,” aliongeza Balozi Avetisyan. 

Tanzania na Urusi zinashirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi, afya, biashara, viwanda, uwekezaji na utalii ambapo kwa pamoja zimekubaliana kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta tija katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi jana jioni (tarehe 14 Juni, 2023) Jijini Dar es Salaam. kushoto ni Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiaana na Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan wakati maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi jana jioni (tarehe 14 Juni, 2023) Jijini Dar es Salaam

Washiriki wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi

Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi jana jioni (tarehe 14 Juni, 2023) Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan akizungumza na washiriki wakati maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi jana jioni (tarehe 14 Juni, 2023) Jijini Dar es Salaam



Wednesday, June 14, 2023

TANZANIA, MISRI KUIMARISHA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kuimarisha ushirikiano wake na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri katika sekta za biashara na uwekezaji.

Hayo yamebainishwa wakati wa mazungumzo baina ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) na Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry walipokutana katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mbarouk amesema kuwa ni wakati muafaka kwa Serikali za Tanzania na Misri kuwekeza zaidi katika sekta ya biashara na uwekezaji ili kukuza uchumi wa mataifa yote mawili.

“Ili kukuza na kuimarisha misingi ya biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Misri tunahitaji kufanya mkutano wa Mkutano wa Tume ya pamoja ya Ushirikiano ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Misri, pamoja na kuanzisha Baraza la biashara ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara wetu kubadilishana uzoefu na mawazo ya biashara na uwekezaji,” alisema Balozi Mbarouk.

Aidha, Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepanga kufanya Mkutano wa Tume ya pamoja ya Ushirikiano ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Misri mwezi Oktoba, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo utajadili mazingira ya biashara na uwekezaji kwa pande zote mbili.

“Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji kwa kuondoa kero mbalimbali zilizokuwa zinawakabili wawekezaji hivyo mazingira ya biashara na uwekezaji ni mazuri na yanaridhisha,” aliongeza Balozi Mbarouk.

Naye Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry alisema kuwa kufanyika kwa JPC ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa Misri na Tanzania katika sekta ya biashara na uwekezaji.

“tumejadili na kukubaliana kuanzisha Baraza la biashara kati ya nchi zetu ili kuweza kuimarisha sekta hiyo kwa maslahi ya pande zote mbili,” alisema Balozi Badry

Balozi Badry aliongeza kuwa Misri imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, maji, nishati, utamaduni, utalii, kilimo pamoja na uvuvi na mifugo, hivyo ni wakati muafaka kwa mataifa hayo mawili kujikita zaidi katika sekta ya biashara na uwekezaji.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimkaribisha Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimsikiliza Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry pamoja na Balozi wa Misri Nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Misri anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Dkt. Mohamed El Badry pamoja na Balozi wa Misri Nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail katika picha ya pamoja na ujumbe wake



BALOZI MBAROUK ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA ITALIA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Italia nchini, kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Mhe. Silvio Berlusconi kilichotokea tarehe 12 Juni, 2023.

Mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Balozi Mbarouk amesema Tanzania inamkumbuka Mhe. Berlusconi kwa kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania Italia enzi za uongozi wake.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Italia nchini, kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Mhe. Silvio Berlusconi



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Italia nchini, kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Mhe. Silvio Berlusconi. aliyesimama ni Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akitoa salamu za pole kwa Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Mhe. Silvio Berlusconi


DKT. TAX , TIC, TTB NA ZIPA WAWASHAWISHI WAFANYABIASHARA WA AUSTRIA WAJE NCHINI


 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza katika Mkutano na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini Vienna.


Kaimu Balozi na mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Umoja wa Mataifa Vienna Bi Elizabeth Rwitunga akizungumza katika Mkutano na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini Vienna.

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme wakifuatilia mkutano kati ya Wizara na Jumuiya ya Wafanyabiashara  Austria jijini Vienna uliofanyika tarehe 13 Juni, 2023.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uwekezaji Zanzibar Bw. Khamis Dunia akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni, 2023
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uwekezaji Zanzibar Bw. Khamis Dunia akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni, 2023.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Gilead Teri akizungumza katika Mkutano na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna.

 











 

 




Waziri wa Mambo ya na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Dkt. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini Vienna na kuwashawishi wafanyabiashara hao waje nchini kuwekeza, kufanya biashara na kutembelea vivutio vya utalii.

 
Dkt. Tax ameshiriki mkutano huo pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ambapo kwa pamoja walielezea jinsi serikali ilivyoboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji nchini waliwashawishi kwamba Tanzania ni salama kwa mitaji yao na waje nchini pia kutembelea vivutio vya utalii


Wamewaelezea Wafanyabiashara wa Austria juu ya faida zinazoweza kupatikana kupitia uwekezaji au ubia na Serikali ya Tanzania au mtu binafsi kwamba hawatajuta kufanya hivyo.

Dkt. Tax amewahakikishia Wafanyabiashara hao kuwa Tanzania ni nchi yenye amani na usalama wake ni wa hali ya juu na hivyo ni kituo muafaka kwao kuwekeza mitaji yao na kufanya biashara na ana hakika watapata soko, faida na kurejesha fedha zao watakazowekeza nchini.


"Tanzania ni nchi yenye amani na usalama, kiufupi Tanzania ni njema na kwa hivyo mtakuwa na uhakika wa kurejesha fedha zenu mlizoweka kwa kuwa na soko la uhakika na faida pia mtapata kutokana na usalama wa mitaji yenu na kufanya biashara,” alisema Mhe. Waziri.


Akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Bw. Khamis Dunia alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefungua milango ya uwekezaji na kuwakaribisha wenye nia ya kuwekeza Zanzibar katika maeneo ya utalii na miundombinu waje nchini kuwekeza na kujionea vivutio.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) amesema Serikali imeunganisha mifumo ya taasisi za usajili na uwezeshaji biashara ili kutoa huduma bora kwa wawekezaji. Taasisi hizo zinajumuisha TIC, NIDA, TRA, BRELA, Uhamiaji na Idara ya Kazi.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Damas Mfugale Ali waambie wafanyabiashara hao kuwa eneo la utalii lina utalii wa aina nyingi ambazo wawekezaji wanaweza kuja nchini na kutembelea maeneo hayo na kuwekeza.


Aliongeza kuwa Wafanyabiashara hao wanaweza pia kuja nchini na kuwekeza mmoja mmoja au kwa kuungana na serikali kwa njia ya ubia na hivyo kusaidia uendelezaji wa maeneo ya utalii kwa faida ya pande zote mbili.

 




VIJANA WA TANZANIA WALIOKUWA KWENYE MAFUNZO YA KILIMO CHA KISASA NCHINI ISRAEL WANG'ARA

Vijana 99 kati ya vijana 100 waliokuwa wanapatiwa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa njia ya vitendo katika Kituo cha Kimataifa cha mafunzo ya Kilimo cha Arava kilichopo Kusini mwa Israel, wamehitimu mafunzo na kutunukiwa vyeti katika mahafali yaliyofanyika tarehe 12 Juni 2023 (The Arava International Center for Agriculture Training - AICAT).


Kundi hili la watu 99 ambaye mmoja alirejeshwa nchini kutokana na changamoto za kiafya ni la kwanza kuhitimu katika kituo hicho tangu Tanzania ilipojiunga kwa mara ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2022/2023.


Katika hotuba yake, Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Alex Kallua aliwapongeza wahitimu wote na kuwaasa kuwa chachu ya mabadiliko wanaporejea nchini kwao kwa kufanyia kazi kwa vitendo mafunzo waliyoyapata nchini Israel.

 

Katika mahafali hayo, mradi mmoja kutoka kwa vijana wa Tanzania ulishinda tuzo ya Dolaza Marekani 6,000.00 kutoka kwa The Dean Family Fellowship Grant, kufuatia shindano la kuandika na kuwasilisha mradi ambao vijana husika watafanya na kuleta mabadiliko chanya kwao na kwa jamii inayowazunguka, mara baada ya kurejea nyumbani. Tuzo hii itawawezesha vijana walioshinda kuanzisha mradi husika na hivyo kujikwamua kiuchumi. Shindano lilihusisha nchi 12 ambazo zinashiriki mafunzo hayo na tuzo ilitolewa kwa nchi 7 ikiwemo Tanzania.

 

Aidha, vijana 5 kutoka Tanzania walipata tuzo ya wanafunzi bora na kijana mmoja ambaye alikuwa kiongozi wa kundi la Tanzania amepewa ofa ya kuendelea na mafunzo kwa mwaka ujao wa masomo kutokana na nidhamu na uongozi uliotukuka.

 

Kwa mwaka wa masomo 2022/2023, Tanzania ilipewa nafasi za masomo 250 ambapo vijana 100 walipelekwa kwenye kituo cha AICAT na 150 walipelekwa kituo cha mafunzo cha Agrostudies ambacho kimekuwa kikitoa mafunzo hayo kwa vijana wa Tanzania tangu programu hii ilivyoanza. Vijana wengine 150 wanatarajiwa kuhitimu mafunzo yao mwezi Agosti 2023.

 

Kwa mwaka wa masomo 2023/2024, Tanzania imepewa nafasi 260 ambapo vijana 150 watapelekwa Agrostudies na vijana 110 watapelekwa AICAT.

Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Alex Kallua akimtunuku cheti mmoja wa mhitimu wa mafunzo ya kilimo kwa vitendo nchini Israel 
Mhitimu wa mafunzo ya kilimo kwa vitendo nchini Israel baada ya kutunukiwa cheti na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Alex Kallua

Wahitimu wa mafunzo ya kilimo kwa vitendo wakiwa na vyetu vyao baada ya kutunukiwa wakati wa mahafali yaliyofanyika nchini Israel tarehe 12 Juni 2023.

Usawa wa kijinsia umezingatiwa, Mhitimu wa Kike wa Mafunzo ya kilimo kwa vitendo nchini Israel akitunukiwa cheti na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Alex Kallua

Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Alex Kallua akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wakiwa wameshikilia mfano wa hundi ya Dola za Marekani 6000 kufuatia ushindi walioupata kwenye shindano la Andiko Mradi




DKT. TAX, TIC, ZIPA & TTB WAZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA VIENNA

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza katika Mkutano na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini Vienna.


Kaimu Balozi na mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Umoja wa Mataifa Vienna Bi Elizabeth Rwitunga akizungumza katika Mkutano na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini Vienna.

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme wakifuatilia mkutano kati ya Wizara na Jumuiya ya Wafanyabiashara  Austria jijini Vienna uliofanyika tarehe 13 Juni, 2023.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Gilead Teri akizungumza katika Mkutano na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna.



Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uwekezaji Zanzibar Bw. Khamis Dunia akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni, 2023.

Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Damas Mfugale akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria uliofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni, 2023
Mmoja wa wafanyabiashara wa nchini Austria akizungumza katika kikao kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wafanyabiashara wa Austria kilichofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni,2023 kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali nchini kwa wafanyabiashara hao

Baadhi ya wafanyabiashara wa nchini Austria walioshiriki mkutano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wafanyabiashara wa Austria kilichofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni,2023 kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali nchini kwa wafanyabiashara hao

 

Baadhi ya wafanyabiashara wa nchini Austria walioshiriki  mkutano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wafanyabiashara wa Austria kilichofanyika jijini Vienna tarehe 13 Juni,2023 kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali nchini kwa wafanyabiashara hao


Waziri wa Mambo ya na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Dkt. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na jumuiya ya Wafanyabiashara wa Austria jijini Vienna.


Dkt. Tax ameshiriki kikao hicho pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ambapo kwa pamoja walielezea jinsi serikali ilivyoboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji nchini.


Wamewaelezea Wafanyabiashara wa Austria juu ya faida zinazoweza kupatikana kupitia uwekezaji au ubia na Serikali ya Tanzania au mtu binafsi.

Dkt. Tax amewahakikishia Wafanyabiashara hao kuwa Tanzania ni nchi yenye amani na usalama na ni kituo muafaka kwao kuwekeza mitaji yao na kufanya biashara.


Tanzania ni nchi yenye amani na usalama, kiufupi Tanzania ni njema na kwa hivyo mna uhakika na usalama wa mitaji yenu na kufanya biashara,” alisema Mhe. Waziri.


Akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Bw. Khamis Dunia alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefungua milango ya uwekezaji na kuwakaribisha wenye nia ya kuwekeza Zanzibar katika maeneo ya utalii na miundombinu waje nchini kuwekeza na kujionea vivutio.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) amesema Serikali imeunganisha mifumo ya taasisi za usajili na uwezeshaji biashara ili kutoa huduma bora kwa wawekezaji. Taasisi hizo zinajumuisha TIC, NIDA, TRA, BRELA, Uhamiaji na Idara ya Kazi.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Damas Mfugale Ali waambie wafanyabiashara hao kuwa eneo la utalii lina utalii wa aina nyingi ambazo wawekezaji wanaweza kuja nchini na kutembelea maeneo hayo na kuwekeza.


Aliongeza kuwa Wafanyabiashara hao wanaweza pia kuja nchini na kuwekeza mmoja mmoja au kwa kuungana na serikali kwa njia ya ubia na hivyo kusaidia uendelezaji wa maeneo ya utalii kwa faida ya pande zote mbili.

 

Tuesday, June 13, 2023

SHIRIKA LA NDEGE LA UFARANSA LAANZA SAFARI ZA MOJA KWA MOJA KUTOKA PARIS HADI DAR

Shirika la Ndege la Ufaransa yaani Air France limezindua safari yake ya kwanza kutoka Paris Charles de Gaulle hadi jijini Dar es Salaam tarehe 12 Juni 2023.

 

Uzinduzi wa safari hizi ni mwendelezo wa huduma za Shirika hilo baada ya kuazisha safari zake za moja kwa moja kutoka Paris hadi Zanzibar mwaka 2021.

 

Kuanzishwa kwa safari hii mpya na Shirika hilo ni matokeo ya jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhamasisha utalii, biashara na uwekezaji nchini . Lakini pia zinatokana na ushirikiano na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Ufaransa.

 

Aidha, inatarajiwa kuwa kuanzishwa kwa safari hizi kutasaidia kuongeza idadi ya watalii, wawekezaji na wafanyabiashara watakaotembelea nchini na hatimaye kukuza uchumi wa nchi.

 

Huduma za usafiri kupitia Air France  zitafanyika mara tatu kwa wiki katika siku za Jumatatu, Jumatano na Jumamosi ambapo Shirika hilo litatumia ndege aina ya Boeing 787-9.

 

Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi walishiriki kwenye mapokezi hayo ambayo pia yalimshirikisha Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui huku Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax kwenye mapokezi hayo.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto) akiwaongoza viongozi wengine kukata utepe kuashiria mapokezi ya ndege ya Shirika la Air France iliyoanza rasmi safari zake kutoka Paris hadi Dar es Salaam tarehe 12 Juni 2023. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab aliyemwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax kwenye mapokezi hayo
Ndege ya Shirika la Air France ikipokelewa kwa kumwagiwa maji baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ikitokea Paris, Ufaransa. Ndege hiyo itafanya safari zake jijini Dar es Salaam mara tatu kwa wiki katika siku za Jumatatu, Jumatano na Jumamosi
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab akizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa  na Ubalozi wa Ufaransa nchini. Hafla hiyo ilifanyika kabla ya mapokezi rasmi ya Ndege ya Air France.
Hafla ikiendelea
Balozi Fatma na Viongozi wengine wakiwemo Mabalozi na Wawakilishi wa Ubalozi wa Ufaransa nchini wakikata keki kuashiria kukaribisha safari za Ndege za Shirika la Air France kutoka Paris kuja Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika kabla ya ndege hiyo kuwasili
Picha ya pamoja