Na
Mwandishi wetu, Dar
Wafanyabiashara
nchini wanaofanya biashara nje ya nchi wameshauriwa kuwasiliana na balozi za
Tanzania ili kupata taarifa sahihi kuhusu fursa za biashara na uwekezaji katika
nchi wanazopenda kufanya nazo biashara.
Wito
huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Joseph Sokoine wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa
ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Balozi
Sokoine amesema kuwa endapo wafanyabiashara watatumia Balozi za Tanzania Nje ya
Nchi itakuwa rahisi kwao kuwapatia taarifa sahihi zaidi kuliko kutumia vyanzo
vingine.
“Endapo
wafanyabiashara wetu wanaofanya biashara nje watatumia fursa ya kuwasiliana na
Wizara ya Mambo ya Nje kupitia Balozi zake Nje ya Nchi watapatiwa taarifa
sahihi ambazo zitawasaidia kuokoa muda na kupata bidhaa kwa wakati,” Amesema
Balozi Sokoine.
Pamoja
na mambo mengine, Balozi Sokoine amewasihi watanzana kwa ujumla kupita katika
banda la Wizara ya Mambo ya Nje ili kuweza kupata uelewa wa taarifa/ufafanuzi
wa masuala mbalimbali ya kidiplomasia.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi
Joseph Sokoine akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya
Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi
Joseph Sokoine akimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Bw. Emmanuel Buhohela katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara
(Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Balozi Mteule, Mhe. Edwin Rutageruka.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi
Joseph Sokoine akiongea na waandishi wa habari katika banda la Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati alipotembelea Maonesho ya 45
ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi
Joseph Sokoine, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade
Balozi Mteule, Mhe. Edwin Rutageruka na Mwakilishi kutoka chuo cha
Diplomasia, Mhe. Balozi Innocent Shio wakiwa katika picha ya pamoja na
watumishi wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara
(Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi
Joseph Sokoine akipata ufafanuzi kutoka banda la magazeti ya Serikali (TSN)
wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea
Jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi
Joseph Sokoine akiwa katika banda la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha
Arusha (AICC) wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara
(Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.