Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kati) amekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Alfa Care Group Limited Bw. Dadkarim Mulla (wa kwanza kushoto) ambaye aliambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo (wa pili kushoto) walipomtembelea Wizarani tarehe 1 Februari 2022 jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Edwin Rutageruka (mwenye tai) na Katibu wa Waziri, Bw. Seif Kamtunda.
Katika Mazungumzo yao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kwa lengo ya kuyafikia malengo ya kitaifa kwa ufanisi.
Vilevile wamejadili namna ya kuongeza uwekezaji katika miradi ya maendeleo husasani sekta ya afya, miundombinu, teknolojia, utalii sambamba na kukuza ajira kwa watanzania. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.