Mhe. Innocent Eugene Shiyo, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Kamisheni Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA) amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe.Dkt. Vera Songwe, Katibu Mtendaji wa Kamisheni Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA).
Wakati
wa hafla hiyo, Mhe. Dkt. Vera Songwe alimpongeza Balozi Shiyo kwa kuteuliwa na
Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi
Afrika (UNECA) yenye Makao Makuu Jijini Addis Ababa, Ethiopia na amemkaribisha na kumtakia
heri katika utekelezaji wa majukumu yake.
Wakati wa mazungumzo yao, Balozi
Shiyo na Dkt. Vera Songwe wamekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo
kati ya Tanzania na UNECA katika masuala ya kipaumbele ikiwemo utekelezaji wa Malengo
ya Maendeleo Endelevu, Mpango wa Maendeleo wa Afrika wa Agenda 2063 na juhudi
za kukwamua uchumi dhidi ya madhara ya UVIKO-19.
Dkt,
Vera Songwe ameeleza utayari wa UNECA kuisadia Tanzania kujenga na kuimarisha
uwezo katika mikakati ya kukuza sekta za utalii,afya, kilimo,sekta binafsi,
ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika
(AfCFTA), mapambano dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi na uwezeshaji Wanawake
kwenye matumizi ya Teknolojia.
Kamisheni
ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika ilianzishwa mwaka 1958 kwa ajili ya kukuza
maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii katika nchi za Afrika, kukuza Mtangamano wa
Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya Afrika.
Mhe. Balozi Shiyo akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Songwe mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.