Konseli Mkuu Bw. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na Konseli Mkuu wa Saudi Arabia Dubai Bw. Bw. Emad A. Madani
Konseli Mkuu wa Tanzania, Dubai, Bw. Omar Mjenga amekutana na Konseli Mkuu wa Saudi Arabia, Dubai, ambaye pia ndio Mkuu Makonseli Wakuu waliopo Dubai (Dean of Diplomatic Corps), Mhe. Emad A. Madani katika ofisi za Koseli Kuu ya Saudi Arabia.
Bw. Mjenga alienda kumtembelea ili kuomba ushiriki wake pamoja na Makonseli Wakuu wote kwenye kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya Utalii nchini Tanzania, litakalofanyika tarehe 17 Disemba 2014.
Bw. Emad Madani amesema atashiriki vikamlifu kwenye kongamano hilo huku akisema kuwa Tanzania na Saudi Arabia ni nchi rafiki wa siku nyingi, na hivyo basi wapo tayari kuomba taasisi ya utalii ya Saudi Arabia kushiriki pia.
Aliahidi kuwaomba Makonseli Wakuu wote washiriki.
Kongamano hilo limeandaliwa na Koseli Kuu ya Tanzania uliopo Dubai kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.