Simu: 255-22-2114615,
211906-12
|
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) ameondoka nchini tarehe
14 Januari 2015 kwenda Urusi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa
mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Mhe. Sergey Lavrov.
Ziara hiyo ya
kwanza ya kikazi ya Waziri Membe nchini Urusi, inalenga kwenye kuimarisha ushirikiano
baina ya Tanzania na Urusi.
Akiwa nchini humo, Mhe.
Membe anatarajiwa kutumia fursa hiyo kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na
Urusi, hususan katika maeneo ya biashara, uwekezaji na ubadilishanaji wa
teknolojia.
Tanzania inaweza
kufaidika na utaalamu wa Urusi katika sekta za uzalishaji wa nishati, uvuvi,
afya, kilimo na huduma za jamii.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
14.01.2015
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.