Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima akizungumza na Balozi wa China nchini, Mhe. Dkt. Lu Youqing alipofika Wizarani kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na China. Katika mazungumzo yao walijadili namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano hususan katika masuala ya kukuza uchumi kupitia viwanda na uwekezaji na kuendelea kukamilisha miradi mbalimbali ya pamoja ikiwemo ule wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.