Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Dkt. Augustine Mahiga kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Balozi Dkt. Amina Mohammed wakisaini Makubaliano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya. Makubaliano hayo yamesainiwa kufuatia Kikao cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JCC) kati ya Tanzania na Kenya kilichofanyika tarehe 1 hadi 3 Desemba, 2016 ambapo masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili yalijadiliwa na kukubaliwa. Masuala ya ushirikiano ni pamoja na kilimo, uchukuzi, utalii, nishati na madini na uvuvi. Hafla hiyo fupi ya uwekaji saini makubaliano hayo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2016. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.