Serikali ya Tanzania na
Cuba zimeahidi kuendelea kuweka mikakati madhubuti kwaajili ya kuimarisha ushirikiano
wa siku nyingi ulioasisiwa na viongozi wakuu wa Mataifa hayo Hayati Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
na Hayati Fidel Castor.
Hayo yamesemwa leo katika
mazungumzo baina ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba na Balozi wa Cuba
nchini, Mhe. Prof. Lucas Domingo Hernandez Polledo walipokutana katika ofisi za
Wizara Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa Mhe. Kolimba
alieleza Cuba imekuwa mdau wa Maendeleo nchini tangu enzi za
ukoloni ambapo ilishiriki katika kupigania Ukombozi wa Tanzania na Afrika kwa
ujumla na hivyo kuleta undugu baina ya watu wa mataifa hayo mawili.
Aidha, aliongeza kwa
kusema “Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua jitihada na mchango
wa Serikali ya Cuba katika Sekta ya Afya kwa kuleta madakatari kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Pia ujenzi wa kiwanda cha viuadudu kilichopo
Kibaha ni sehemu ya jitihada za kuwasaidia Watanzania katika kuhakikisha
wanakuwa na Afya bora ili kuweza kumudu majukumu yao ya kila siku katika
kuliletea Taifa maendeleo” alisema Dkt. Kolimba.
Halikadhalika Mhe. Prof. Polledo
alisisitiza kuwa Cuba itaendeleza ushirikiano na Tanzania na kuzidi kuangalia
maeneo mengine ya ushirikiano hususani upande wa michezo ambapo nchi hiyo
imekuwa ikifanya vizuri katika mchezo wa ngumi pamoja na walimu stadi wa mchezo
huo ambao wamekuwa wakitoa mafunzo katika mataifa mengine ya Afrika.
Pia alieleza kutambua
mchango wa Tanzania katika Kikao cha 72 cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa msimamo
wake wa kutaka Cuba kuondolewe vikwazo vya kiuchumi ambavyo vimekuwa
vikikwamisha na kurudisha nyuma jitihada za maendeleo ya Taifa hilo. “ ni
wakati sasa Cuba na Tanzania zikaimarisha ushirikiano wake kwa kuhakikisha unakuwa
na mafanikio kiuchumi kwa manufaa ya
mataifa hayo” alisema Prof. Polledo
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.