Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Ushirikiano kati ya Tanzania na China katika sekta ya afya ambapo Dkt. Mahiga ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Afya, ambapo imeendelea kuleta Madaktari wakujitolea katika Hospitali mbalimbali zilizopo nchini zikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Aidha, Tanzania na China zimekuwa na mahusiano katika sekta ya Afya, tangu mwaka 1968 ambapo madaktari kutoka jimbo la Shandong wamekuwa wakija Tanzania kutoa Huduma za Afya katika mikoa mbalimbali nchini.
Madhimisho hayo yalihudhuriwa na Dkt. Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalim,
maadhimisho hayo yamefanyika katika Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China nchini. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.