Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Bernard Archiula mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika chuo hicho. Mhe. Naibu Waziri aliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya chuoni hapo pamoja na kufanya mkutano na Uongozi wa chuo na Wakufunzi. Katika mkutano huo, uongozi wa chuo pamoja na Wakufunzi walitumia fursa hiyo kumwelezea Dkt. Ndumbaro changamoto wanazokabiliana nazo chuoni hapo ikiwa ni pamoja na ufinyu wa majengo kulingana na mahitaji ya chuo na uchache na uchakavu wa miundombinu ya kufundishia.
Aidha, Mhe. Naibu Waziri alitumia ziara hiyo kujua mikakati mbalimbali waliyojiwekea chuoni hapo ikiwa ni pamoja na dhamira ya kujenga majengo mapya ambayo ramani ya mchoro wa majengo hayo iliwasilishwa kwa Mhe. Naibu Waziri.
Kwa Upande wa Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kuupongeza Uongozi pamoja na Wakufunzi wa chuo cha Diplomasia kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na changamoto wanazokumbana nazo. Aidha, alitoa rai kwa Uongozi wa Chuo pamoja na Wakufunzi wawe wabunifu zaidi. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.