Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro
(Mb) amesaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini kufuatia
kifo cha Rais wa Taifa hilo Pierre Nkurunziza aliyefariki Juni 08, 2020.
Akizungumza
mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi ubalozi wa Burundi nchini, Jijini Dar es Salaam Dkt. Ndumbaro ametoa pole kwa wananchi wote wa Burundi na kuwasihi kuendelea
kuwa watulivu na wastahimilivu wakati huu wa msiba.
"Kusaini
kitabu cha maombolezo ni ishara ya ushirikiano wetu, umoja wetu na undugu wetu
na ndugu zetu wa Burundi. Kifo cha Rais Nkurunzinza kinawahusu pia watanzania
kwa sababu Rais Nkurunzinza ni Rais aliyekuwa karibu sana na Tanzania kuliko
nchi nyingine yeyote ile, lakini pia Burundi ipo karibu sana na Tanzania,
Amesema Dkt. Ndumbaro.
Naibu
Waziri, Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa, Pengo la Rais Nkurunzinza ni pengo kubwa
sana kwa watanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Afrika kwa ujumla.
Nae
Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Gervais Abayeho, amemshukuru Naibu Waziri wa
mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro kwa kufika
kwake kuhani msiba huo na kuongeza kuwa hali hiyo inaonesha upendo ambao unaendelea
kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili.
Aidha,
Serikali ya Burundi kupitia ubalozi wake hapa nchini, imetoa mualiko kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa kushiriki
mazishi ya Rais Nkurunzinza yanayotarajiwa kufanyika Alhamisi tarehe 18 Juni
2020 nchini Burundi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro
(Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini leo Jijini
Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akisaini
kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto kwake ni Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Gervais Abayeho.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akisaini
kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto kwake ni Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Gervais Abayeho.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.