Na Mwandishi wetu, Roma
Ubalozi
wa Tanzania nchini Italia umekutana na kufanya Mkutano Mkuu na Jumuiya mbalimbali
za Watanzania wanaoishi maeneo mbalimbali nchini Italia (Diaspora) kwaajili ya kuimarisha
mahusiano na ushirikiano baina ya pande mbili.
Akifungua
mkutano huo mwishoni mwa wiki, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud
Thabit Kombo alitoa wito kwa Watanzania
hao kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuiletea Tanzania maendeleo.
“Nawashauri kujisajili katika daftari la Diaspora wa Italia ili kuwa na
takwimu na kumbukumbu sahihi za Watanzania waliopo Italia. Takwimu na
kumbukumbu hizi zitasaidia Ubalozi kuwaunganisha Wanadiaspora na wabia wa
maendeleo ambao wana nia au tayari wanaendesha shughuli zao nchini Tanzania na
wanahitaji kushirikiana na Diaspora,” Amesema Balozi Kombo.
Pamoja
na mambo mengine, mkutano huo ulijadili masuala mbalimbali yanayowahusu wanadiaspora
ikiwemo changamoto za kiutendaji na ushirikiano katika Jumuiya zao ambazo zilianishwa
wazi kwenye taarifa za kiutendaji zilizowasilishwa na Viongozi wa Jumuiya.
Mkutano uliazimia kuendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina ya
Wanadiaspora na Ubalozi kwa kuanisha mkakati thabiti wa kuboresha mawasiliano
baina ya pande mbili.
Aidha, wanadiaspora hao wameahidi kuendelea kushirikiana na Ubalozi wa
Tanzania nchini Italia katika kuiletea
nchi yao maendeleo kwa kuwekeza nchini kwao. Kadhalika, Ubalozi umeahidi kutafuta
suluhu ya kudumu dhidi ya changamoto zinazowakabili wanadiaspora waishio nchini
Italia.
Mkutano
huo ulihudhuriwa pia na wanadiaspora takriban 100 akiwemo Mhashamu Baba Askofu Mkuu
Protase Rugambwa, Katibu Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu.
Nchini
Italia zipo Jumuiya sita zinazotoka maeneo ya Roma, Napoli, Modena Central
North, Genova, Modena na Umoja wa Watanzania Wakatoliki unaojumuisha Waklero, Watawa, Waseminari na walelewa wa Utawa wanaofanya kazi za kitume
hapa Italia.
Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud
Thabit Kombo akiongea na Wanadiaspora (hawapo pichani) wanaoishi nchini Italia wakati wa Mkutano
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma akiwasilisha Bi.
Anastacia Lubangila, taarifa ya Jumuiya hiyo wakati wa mkutano
Mhashamu
Baba Askofu Mkuu, Protase Rugambwa akifuatalia majadiliano
Mwenyekiti
Kamati Kuu ya Wanadiaspora Italia Bw. Maulid Kagutta, akiwasilisha taarifa ya
Diaspora Italia
Balozi Kombo akipokea picha ya nembo rasmi ya Jumuiya ya Watanzania Genova kutoka kwa
Bi. Eva Nangela, Mwenyekiti wa Jumuiya (kushoto). Wanaoshuhudia (kulia) ni Bi.
Zakia Kombo, Mwenza wa Mhe. Balozi; Baba Askofu Mkuu Rugambwa na Maafisa Ubalozi,
Bw. Sigfried Nnembuka pamoja na Jacqueline Mbuya.
Wanadiaspora wakifuatilia mkutano
Wanadiaspora wakifuatilia mkutano
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.