|
Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alipowasili katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia jijini Riyadh na kuzungumza na watumishi wa Ubalozi huo.
|
|
Balozi Liberata Mulamula (katikati) akiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (kulia) wakiangalia picha ukutani (hazipo ktika picha) walipowasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Riyadh kwa ajili ya kukagua ubalozi huo na kuzungumza na watumishi.
|
|
Balozi Liberata
Mulamula (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali
Mwadini (wa kwanza kulia) huku Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza (kushoto) akifuatilia mazungumzo hayo.
|
|
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali
Mwadini (kulia) akiwaonesha kitu Balozi Liberata
Mulamula (katikati) na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba
Ndaki (kushoto) walipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Riyadh . |
|
Balozi Liberata
Mulamula akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Riyadh alipotembelea na kuzungumza na watumishi wa Ubalozi. |
|
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba
Ndaki (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia walipotembelea Ofisi hizi jijini Riyadh . |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia alipotembelea Ofisi hizo jijini Riyadh.
|
|
kikao kikiendelea katika Ofisi za Ubalozi jijini Riyadh
|
|
Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
(katikati) katika picha ya pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi
Arabia alipotembelea Ofisi hizo jijini Riyadh. |
|
Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
(katikati) katika picha ya pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi
Arabia alipotembelea Ofisi hizo jijini Riyadh. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania
nchini Saudi Arabia nchini humo.
Akizungumza
na Watumishi wa Ubalozi jijini Riyadh, Balozi Mulamula amewataka kuzingatia
ulinzi wa taswira ya nchi yao hasa kwa kuzingatia mienendo ya maisha yao na
kauli zao pia.
“Chochote mnachofanya ndio sura na kioo cha Jamhui
ya Muungano wa Tanzania huku, nawaombeni sana kuzingatia hilo, japo ni kweli
kwa mienendo yenu hatuwaingilii lakini hamna budi kujua kuwa nyie ni taswira ya
nchi yetu huku,” alisema Balozi Mulamula.
Balozi Mulamula pia amewataka watumishi hao
kuhakikisha wanafuata na kuzingatia misingi na kanuni za utumishi wa umma licha
ya kutekeleza majukumu yao nje ya Tanzania.
Pia amewataka Mabalozi na watumishi walioko katika
balozi za Tanzania kuendela kuwa walezi wa Watanzania popote walipo na kuwa
tayari kuwasaidia pale watakapohitaji msaada kutoka katika balozi hizo.
Waziri
Mulamula yuko nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan
Al Saud, alioutoa mwezi Machi 2021 alipotembelea Tanzania na anataarajia
kurejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.
Katika ziara hiyo Waziri Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki , kituo cha Uwekezaji nchini na Chama cha cha wafanyabiashara na wenye viwanda nchini (TCCIA)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.