Waziri wa Uingereza anayeshughulikia Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford akionesha zawadi ya picha ya michoro ya tingatinga ambayo alipewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula walipokutana kwa jijini Dodoma. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kushoto) akitoa maelezo kuhusiana na michoro ya picha ya tingatinga ambayo alimpatia Waziri wa Uingereza anayeshughulikia Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford walipokutana jijini Dodoma |
Balozi Liberata Mulamula (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford ambaye alifika jijini Dodoma kwa ziara ya kikazi nchini tarehe 03 Aprili 2022. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku tatu kuanzai tarehe 3-5 Aprili 2022.
Katika mazungumzo yao viongozi hao wamekubaliana kuendelea kushirikiana na kuimarisha uhusiano mzuri ulioko baina ya Tanzania na Uingereza.
Balozi Mulamula amemshukuru Mhe. Ford kwa uamuzi wa kuja kuitembelea Tanzania na kujionea utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo inafadhiliwa na Uingereza na kumualika kuja tena nchini wakati mwingine.
Naye Mhe. Ford ameelezea kufurahishwa ridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo jambo ambalo amesema inatia moyo kuona fedha zinazotolewa na nchi hiyo zinafanya kazi iliyokusudiwa na hivyo kusaidia harakati za kubadili maisha ya Watanzania.
Waziri Ford aliwasili nchini kupitia uwanja wa Ndege wa Kimataifa ya Kilimanjaro ambako alitembelea miradi ya maendeleo katika mji wa Moshi na baadaye jijini Dodoma ambako alikwenda Ikulu ya Chamwino na kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .
Tarehe 04 Aprili 2022, Mhe. Ford atatembelea miradi ya kituo cha afya EngenderHealth Tanzania kilichopo Yombo, kituo cha kuzuia biashara ya binadamu na ulinzi wa watoto vya Jijini Dar es Salaam na kuzindua mradi wa maendeleo wa elimu bunifu nchini unaoitwa Shule Bora utakaofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Jioni ya tarehe 04 Aprili 2022 Mhe. Ford atakuwa na mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea ziara yake nchini na anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 05, Aprili 2022
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.