Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 22, 2024 ameshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa ngazi ya juu wa Wakuu wa Nchi na Serikali ‘Summit of the Future’ uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Umoja wa Mataifa New York nchini Marekani.
Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa nchi na Serikali duniani ili kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo na namna wanaweza kuboresha hali ya sasa na kuzilinda siku zijazo.
Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Waziri Mkuu aliambatana na viongozi waandamizi wa Serikali wakiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Hussein Kattanga.
Mheshimiwa Majaliwa yupo nchini Marekani kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79).
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.