Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, amefanya ziara rasmi katika Ubalozi wa Tanzania jijini Lilongwe, Malawi, kwa lengo la kukagua miundombinu ya ubalozi huo, kupokea taarifa za maendeleo, na kusikiliza changamoto zinazokabili shughuli za kidiplomasia.
Katika ziara hiyo, Mhe.
Kombo alikutana na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Agnes Kayola, pamoja
na maafisa wa ubalozi, ambapo alipokea taarifa kuhusu hali ya mahusiano ya
kidiplomasia, uchumi, siasa, na usalama kati ya Tanzania na Malawi.
Taarifa hiyo ilihusisha pia masuala ya mali za Serikali ya Tanzania zilizopo nchini Malawi, ustawi wa watumishi wa ubalozi, na mchango wa Watanzania waishio Malawi katika maendeleo ya taifa.
Aidha, Waziri Kombo alipokea maelezo kuhusu fursa mbalimbali zinazoweza kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili, hususan katika uwekezaji, biashara za mpakani, na sekta ya utalii.
Akizungumza na maafisa
wa ubalozi, Mhe. Waziri alisisitiza umuhimu wa kuitangaza vyema Tanzania
kimataifa na kutumia fursa zilizopo kwa manufaa ya maendeleo ya taifa. Alitoa
wito kwa Watanzania waishio Malawi kushirikiana na ubalozi katika kukuza
uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi, na kijamii kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake, Balozi Agnes Kayola alimshukuru Waziri Kombo kwa ziara yake na kuahidi kuwa ubalozi utaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa maslahi ya Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) (katikati) akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini malawi Balozi Agness Richard kayola (kushoto) na Mkuu wa Utawala (HOC) Bw. David Fupi (kulia).
Mkurugenzi idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ali Sakila Bujik