Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mhe. Nabil Fahmy (hayupo pichani) katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) Jijini Dar es Salaam. Mhe. Fahmy yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 21 hadi 23 Februari, 2014. Wakati wa mazungumzo hayo masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan katika nyanja za elimu, afya na uwekezaji. Kulia kwa Mhe. Membe ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.