Friday, April 25, 2014

Katibu Mkuu azungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Jimbo la Guangdong


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Mhe. John Haule akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Serikali ya Jimbo la Guangdong la nchini China, Mhe. Liu Xiaojie mara baada ya Naibu Katibu Mkuu huyo kuwasili Ofisini kwake kwa mazungumzo hivi karibuni. Anayeshuhudia katikati ni Bi. Bertha Makilagi, Afisa Mambo ya Nje katika Idara ya Asia na Australasia.
Mhe. Haule akizungumza na Mhe. Liu kuhusu ushirikiano kati ya Jimbo la Guangdong na Serikali ya Tanzania. Masuala ya ushirikiano yaliyozungumzwa ni pamoja na biashara, uwekezaji na utalii. Aidha, Mhe. Haule alimweleza azma ya Tanzania ya kufungua Ubalozi Mdogo mjini Guangzhou.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akiwa na mwakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu, Mhe. John Haule na Naibu Katibu Mkuu wa Serikali ya Jimbo la Guangdong.
Baadhi ya wajumbe waliofuatana na Mhe. Liu, Naibu Katibu Mkuu wa Jimbo la Guangdong la nchini China.
Katibu Mkuu, Mhe. Haule akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na Mhe. Liu na ujumbe wake kama wanavyoonekana pichani.
Mhe. Liu nae akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John Haule (hayupo pichani).
Mhe. Haule na Mhe. Liu katika picha ya pamoja na wajumbe wengine kutoka China na Tanzania.
Mhe. Haule akiagana na mgeni wake Mhe. Liu mara baada ya mazungumzo yao.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.