TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
amefanya uteuzi wa Mabalozi ili kujaza nafasi zilizoachwa
wazi na Mabalozi wastaafu kwa mujibu wa sheria.
Mabalozi
wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:
Balozi
Dora Mmari Msechu, ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Stockholm, Sweden. Hadi uteuzi huu unafanyika Balozi Dora Mmari Msechu ni
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa. Anachukua nafasi ya Balozi Mohamed M.H. Mzale ambaye
amestaafu.
Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba,
ameteuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Moscow, Urusi. Hadi
utaeuzi huu unafanyika, Lt. Gen. Wynjones Matthew Kisamba alikuwa Mkuu wa
Utendaji Kivita na Mafunzo, Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Anachukua nafasi ya Balozi Jaka Mwambi.
Umetolewa na
(John M. Haule)
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
15 APRILI, 2014
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.