Picha na Habari na Reginald Philip
Wizara ya Mambo ya Nje yaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule, amewataka wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na watanzania wote kwa ujumla kutumia nishati endelevu badala ya kuni na mkaa, kuunga mkono juhudi za serikali za kunusuru mazingira.
Akiongea katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyoandaliwa na wizara kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, Bw. Haule alisema hatua nyingine za kutunza mazingira ni kupanda miti; kutolima kwenye miteremko ya milima; kupunguza matumizi makubwa ya mbolea na kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki isiyiteketezeka kwa urahisi.
Wawekezaji katika viwanda watumie teknolojia ya kisasa isiyoongeza gesi joto, alishauri.
Katika maadhimisho hayo chini ya kauli mbiu isemayo “Sayari ya dunia ni kisiwa chetu wote kwa hivyo tuunganishe nguvu zetu kulinda kisiwa hiki,” Bw. Haule alipanda mti kuanzisha mpango wa wizara wa kupanda miti kutunza mazingira. Miti saba ilipandwa nje ya ukumbi wa Julius Nyerere leo kwa kuanzia.
Maadhimisho hayo pia yalishirikisha wafanyakazi wa AICC na ukumbi wa Julius Nyerere.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.