Wednesday, September 10, 2014

Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Rwanda nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Sagore Kayihura. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 09 Septemba, 2014.
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Kayihura mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard K. Membe (Mb.)-kushoto) akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Rais Kikwete na Balozi Kayihura (hawapo pichani)
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Kayihura pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Ubalozi wa Rwanda hapa nchini.
Balaozi Kayihura akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu, Dar es Salaam kabla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais.
Balozi Kayihura akisikiliza wimbo wa taifa lake mara baada ya kuwasili Ikulu. Wengine katika picha ni Balozi Mohammed Maharage Juma (kulia), Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki pamoja na Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.

Bendi ya Polisi ikiongozwa na ASP Kulwa ikipiga wimbo wa taifa kwa heshima ya Balozi Kayihura wa Rwanda nchini (hayupo pichani)

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.