Monday, September 8, 2014

Waziri Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Mabalozi wapya wa Rwanda na Norway hapa nchini



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mpya wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Eugene Sayore Kayihura. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofinini kwa Mhe. Membe tarehe 08 Septemba, 2014.
Waziri Membe akizungumza na Balozi Kayihura mara baada ya kuwasilisha Nakala za hati za utambulisho. Katika mazungumzo hayo Mhe. Membe alimhakikishia ushirikiano Balozi huyo na kumwomba awe huru katika kutekeleza majukumu yake ya kazi wakati wote akiwa hapa nchini.
Balozi Kayihura akiwa na Maafisa Waandamizi wa Ubalozi wa Rwanda hapa nchini aliofutana  nao. Katikati ni  Bw. Sano Lambert na  Bw. Ernest Bugingo.
Mhe. Membe akimsikiliza Balozi Kayihura wakati wa mazungumzo yao.
Mhe. Membe akiagana na Balozi Kayihura.


.................Mhe. Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Norway nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Norway hapa nchini, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad. Hafla hiyo ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Waziri tarehe 08 Septemba, 2014.
Mhe. Membe akizungumza na Balozi Kaarstad mara baada ya kupokea Nakala za hati za utambulisho za Balozi huyo

Balozi Kaarstad na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo pichani)
Mhe. Membe akiagana na Balozi Kaarstad.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.