WAZIRI
MAHIGA AHIMIZA UMUHIMU WA SOMO LA UMOJA WA MATAIFA
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine mahiga amependekeza ni
vema somo la Umoja wa Mataifa likaingizwa katika mitaala ya masomo, ameeleza
hayo alipokuwa akihutubia katika kilele
cha Maadhimisho ya 71 ya Siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo katika
Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kilele
cha maadhimisho hayo Waziri Mahiga alisema “Maadhimisho haya ni muhimu kwa historia ya nchi yetu kwakua yanawezesha
vizazi vyetu kuelewa historia ya nchi yetu na Shirika la Umoja wa Mataifa tangu
kupatikana kwa Uhuru hivyo ni vyema Walimu na Wadau wote katika Sekta ya Elimu
wakatilia mkazo umuhimu wa somo la Umoja wa Mataifa katika shule zetu za Msingi
na Sekondari.”
Vilevile ameeleza umuhimu
na mchango wa Shirika la Umoja wa Mataifa kwa Tanzania na kwa nchi wanachama wengine wa Umoja huo ni
pamoja na kutengeneza agenda ya kimataifa ya maendeleo; kuleta amani hususan
baada ya vita ya kwanza na ya pili ya
Dunia; vilevile Shirika hilo limekuwa likiendelea kuhakikisha amani na Ulinzi inapatikana
katika mataifa yenye migogoro ambapo Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimekuwa
zikishiriki katika masuala ya ulinzi wa amani katika baadhi ya mataifa kama
Lebanon, Sudan Kusini (Dafur) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Pamoja na hayo ameeleza
kuwa kupitia shirika la umoja wa Mataifa Tanzania imefanikiwa kuwa na wawakilishi wa mashirika yote ya Umoja wa
Mataifa ambao pamoja na shughuli nyingine za mashirika hayo yamekuwa
yakifadhili na kushiriki katika shughuli za maendeleo ambapo wastani wa bilioni
za fedha za miradi ya maendeleo zimekuwa zikitolewa kwaajili ya miradi ya
maendeleo. Vilevile Mahakama ya Umoja wa mataifa ya mauaji ya kimbari iliamuriwa
kujengwa nchini Tanzania ambapo makao makuu yake yapo Jijini Arusha licha ya
kumalizika kwa kesi majengo pamoja na nyaraka zote zilizokuwa zikitumika
zimeendelea kubaki nchini kama kumbukumbu za marejeo.
Naye Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez alieleza umuhimu wa ushirikiano katika
kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs), umuhimu wa
kutunza amani na kuheshimu haki za binadamu sambamba na usawa wa jinsia.
Maadhimisho hayo
yalihudhuriwa na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa
yanayowakilisha nchi zao hapa nchini. Wengine ni wadau wa maendeleo kutoka
Sekta binafsi na taasisi za Serikali.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.