Balozi wa Tanzania katika Nchi za Nordic na Baltic mwenye makazi yake Sweden, Mhe. Dora Msechu wa pili kutoka kulia akikata utepe kuashiria uzinduzi wa zoezi la kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera lilifanyika Stockholm, Sweden. Hafla hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Sweden kwa lengo la kuhamasisha Watanzania waishio Sweden kuchangia Wahanga wa Maafa ya tetemeko la ardhi Mkoani Kagera. Zoezi hili maalum la kuchangia maafa linaendelea mpaka tarehe 4 Novemba, 2016 na michango itakayopatikana itakabidhiwa kwa Mhe. Balozi Dora Msechu |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.