ZIARA YA KIKAZI NCHINI TANZANIA YA MHE. IDRISS DEBY ITNO, RAIS WA JAMHURI YA
CHAD NA MWENYEKITI WA UMOJA WA AFRIKA
TAREHE 27-28 NOVEMBA, 2016
Mheshimiwa Idriss Deby Itno, Rais wa Jamhuri ya Chad na Mwenyekiti wa sasa wa
Umoja wa Afrika atakuwa na Ziara ya Kikazi nchini Tanzania tarehe 27-28
Novemba, 2016.
Mheshimiwa Rais Deby atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam tarehe 27 Novemba 2016 saa 8:00 mchana na
kulakiwa na Mwenyeji wake Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muugano wa Tanzania. Aidha, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi wengine waandamizi
wa Serikali ya Tanzania watakuwepo uwanja wa Ndege katika mapokezi hayo.
Akiwa hapa nchini, Mheshimiwa Rais Deby na Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watakuwa na mazungumzo rasmi
Ikulu, ambapo watapata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali
yanayohusu Ukanda wa Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika kwa ujumla.
Mheshimiwa Rais Deby ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa Mwaka 2016-2017,
kipindi ambacho Umoja huo umeendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali
barani Afrika, zikiwemo ugaidi, amani na usalama, na changamoto za
maendeleo.
Ujumbe wa Rais wa Chad unawajumuisha Mke wa Rais Mama
Hinda Deby Itno, Mheshimiwa Moussa Faki Mahamat, Waziri wa Mambo ya Nje,
Mtangamano wa Afrika, na Ushirikiano wa Kimataifa na viongozi wengine
waandamizi wa Serikali ya Chad.
Imetolewa na: KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA
USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
27 NOVEMBA, 2016
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.