Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Zambia nchini, Mhe. Judith Kapijimpanga alimpomtembelea leo Wizarani Jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili. Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni kuhusu kuboresha na kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji inayoziunganisha Tanzania na Zambia, na masuala ya mazingira hasa kwa upande wa Ziwa Tanganyika. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.