Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Suzan Kolimba (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI (UNAIDS), Bw. Dr. Leo Zekeng ofisini kwake jijini Dar Es Salaam leo. Katika mazungumzo hayo, Dkt. Zekeng alisifu jitihada zinazofanywa na Tanzania katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi ambazo zimesaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 25 na pia idadi ya watoto wanaozaliwa na virusi vya ukimwi imepungua kwa kiasi kikubwa. Dkt. Zekeng alisema kuwa kutokana na mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Bi Michel Sidibe anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini mwezi Oktoba 2017 |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.