Friday, May 18, 2018

Balozi Dkt. Possi awasilisha Hati za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye anawakilisha pia na Vatican, Mhe. Dkt. Abdallah Saleh Possi, akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis, Vatican tarehe 17 Mei 2018. 

Kabla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na viongozi muhimu wa Vatican, wakiwemo Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na ushirikiano wa kimataifa, Askofu Mkuu Angelo Becciu, Katibu Mkuu Msaidizi wa Vatican.

Mabalozi wengine waliowasilisha Hati za Utambulisho ni pamoja na Balozi Ahmad Naseem Warraich kutoka Pakistan, Balozi Risto Piipponen kutoka Finland, Balozi Lundeg Purevsuren kutoka Mongolia, Balozi RetÅ¡elisitsoe Calvin Masenyetse kutoka Lesotho, Balozi Karsten Vagn Nielsen kutoka Denmark,  na Balozi Sulaiman Mohammed kutoka Ethiopia. 

Baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Vatican. Katika kikao hicho, Dkt. Possi aliwaeleza Watanzania hao kwamba wana jukumu kubwa la kutumia.nafasi zao kuhakikisha nchi ya Tanzania inadumu katika misingi ya uadilifu, umoja, na amani ambavyo ni misingi muhimu ya maendeleo.

Balozi Dkt. Possi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.

Balozi Dkt. Possi na Mama Balozi, Bi. Sada Mshana, katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Picha kwa hisani ya Vatican


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.