Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Grace Mujuma amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi za Afrika wanao wakilisha nchi zao hapa nchini,Mabalozi hao ni kutoka nchi za Namibia na Malawi, pamoja na mambo mengine katika mazungumzo hayo walijadiliana kuhusu maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Umoja wa Afrika.
Umoja huo ulioanzishwa Mwaka 1963 kwa lengo la kutetea maslahi mbalimbali ya Bara la Afrika, kuongeza umoja zaidi katika kutetea uhuru na kulinda mipaka yake. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.