Na Mwandishi Wetu, Geita
Makamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amewaongoza wakazi wa
Geita na mikoa jirani kuaga mwili wa
aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Pombe
Magufuli katika uwanja wa Magufuli Chato mkoani Geita.
Akizungumza katika shughuli hiyo ya
kuuaga mwili wa hayati Magufuli Wilayani Chato, Makamu wa pili wa Rais wa
Zanzibar ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya mazishi kitaifa amewasihi
Watanzania kuendelea kushikamana katika kulijenga taifa, ambalo Magufuli
ameliacha salama na lenye heshima.
Makamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar, amesema ni wajibu wa viongozi na Watanzania
kuungana kuenzi mazuri yote aliyofanya Hayati Magufuli na kuendeleza sera zake
za kuchapa kazi, kupiga vita rushwa na ubadhirifu na kuweka mbele uzalendo na
maslahi ya taifa.
Mazishi
ya Hayati Dkt. Magufuli yatafanyika Ijumaa Machi 26, 2021 katika makaburi ya
familia kijijini kwake Chato mkoani Geita.
Mawaziri
mbalimbali pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali wakiwa katika uwanja wa
Magufuli tayari kwa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa
Magufuli Chato mkoani Geita
Katibu
wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi-Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed
Said akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika uwanja wa Magufuli wakati
wa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Bashiru Ally akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika
uwanja wa Magufuli wakati wa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani
Geita
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa
Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato
mkoani Geita
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa
Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato
mkoani Geita
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
ya Chato kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
ya Chato kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.