Na mwandishi wetu, Dar
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula apokea nakala ya barua za utambulisho za Makonseli Wakuu wawili kutoka
Msumbiji na Oman wenye makazi Zanzibar.
Makonseli
hao ni Mhe. Agustinho Abacar Trinta Konseli Mkuu wa Msumbiji pamoja na Mhe.
Said Salim Al Sinawi Konseli Mkuu wa Oman
Pamoja
na mambo mengine, viongozi hao wamedajiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha
uhusiano wa Kidiplomasia na Kiuchumi baina ya nchi zao na Tanzania.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula akipokea nakala ya barua za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa
Msumbiji mwenye makazi Zanzibar Mhe. Agostinho Abacar Trinta katika Ofisi ndogo
za Wizara jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula akizungumza na Konseli Mkuu wa Msumbiji mwenye makazi Zanzibar Mhe.
Agostinho Abacar Trinta katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam mara
baada ya kuwasilisha nakala ya hati za utambulisho
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula akipokea nakala ya barua za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Oman
mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi. Uwasilishwaji wa hati hizo
umefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Konseli
Mkuu wa Oman mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi akizungumza na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata
Mulamula katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam mara baada ya
kuwasilisha nakala ya hati za utambulisho
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.