mazungumzo yakiendelea |
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana na kufanya mazungumzo na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (Miss East Africa beauty Pegeant) ofisini kwake jijini Dodoma.
Waandaaji hao ni bi
Jolly Mutesi ambaye ni makamu wa Rais anayetokea nchini Rwanda na bi Mariam
Ikoa ambaye ni muandaaji wa kimataifa anayetokea Tanzania.
Katika mazungumzo hayo na waandaaji hao wa mashindano ya urembo kwa
nchi za Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk amewapongeza waandaaji hao kwa kuja na wazo hilo pamoja na kutaka kufahamu miongozo na
itifaki za kufuatilia ili kufanikisha mashindano hayo.
Akizungumza katika
kikao hicho Mratibu wa mashindanoo hayo Bi Mariam Ikoa amemuelezea Mhe. Naibu
Waziri Mbarouk kwamba ujio wao Wizarani una lengo la kujitambulisha pamoja na kupata
miongozo na itifaki za jinsi ya kuendelea na taratibu za mashindano hayo ya
urembo kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
Amesema mashindano hayo yamepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe
26 Oktoba hadi Novemba 20 2021
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.